[wanabidii] TUSIWE MALOFA WA KWELI!

Tuesday, September 08, 2015
Kwa mtazamo wangu muda wa miezi 2 kwa kampeni za Uchaguzi wa Urais, Ubunge na Madiwani ni mwingi mno. Nilitoa hoja hii mahali fulani na wakaniambia Tanzania ni kubwa mno na miundo mbinu yake ya usafiri ni duni. Hivyo muda mwingi unatakiwa ili wagombea wazunguke kote. Baadae nikauliza una ILANI CHA UCHAUGUZI WA VYAMA VINAVOSHIRIKI? Wengi walijibu hawana. Nikawaambia Ilani ya vyama vingi haizidi uk 30. Vingine 12 nk. Je wanahitaji kweli miezi 2? Na ni je ni vyama vingapi vinavyoweza shiriki kuzunguka nchi nzima? Wakasema labda 2 tu. Vingine vinaaishia kwenye kata kadhaa za KANDA fulani tu.
Siku hizi kuna vyombo vingi vya mawasiliano. Kuna Tv, Radio, Simu, kwa wale walioneemeka skype, Cyber, Twitter nk. Lakini muhimu TV na RADIO. Kwa nini wagombea na kila chama kisitumie njia hizi kunadi sera zao badala ya kupoteza muda wa watu na kutafuna KODI za Watanzania bila sababu. Kipindi hiki cha Kampeni za uchaguzi Nchi imesimama. Huduma nyingi hasa Elimu na Afya ni kama hamna, Kisa fedha ZIPO kwenye Kampeni.

Nadhani aliyesema "Watanzania" kuna walofa na wapumbavu wanaotumia muda wao mwingi kukesha kampeni za vyama vya siasa badala ya kufanya kazi ni sahihi. Wengine juzi tumesikia wameganyagana, kuumia hadi kufa. Kisa kusikiliza au kumuona mgombea. Kwa nini wasiandike kwenye sera zao kwenye magazeti tusome au wasambaze vitabu vya sera zao kisha tuwaulilze maswali badala ya kutumia miezi 2. kutumia hela ovyo? Kwenye mikutano yao naona ni kelele tu, na muziki. Wananchi hawapewi nafasi ya swali bali kuambiwa vitu vya uwongo tu nao wanashangilia kama ZUZU. Wanaambiwa uwongo kuwa kila kitu kitakuwa bure, kwa vile ni malofa na wapumbuva wanashangilia kwa nguvu ndiyoooooooooooo. Mimi sioni kipya tena kwenye Kampeni. Jipya ninaloona ni matusi na kejeli kwa wengine. Na chanzo cha haya yote ni kuwa na muda mwingi mno wa Kampeni.

Tunapoteza mafuta mengi. Angalia misafara ya waheshimiwa hawa. Magari ni mengi mengi mengi. Umeme wanaotumia kuendesha mitamba ni mkubwa kupita kiasi. Watu wengi hawazalishi tena kisa kuwa na vikao vingi kuandaa mikutano hii. Tanzania mwaka kesho ni wa njaa maana watu hawana nafasi ya kulima maana muda mwingi wapo kwenye mikutano ya Uchaguzi. Kwangu mimi huu ni UPUMBAVU NA ULOFA. Mpaka unakufa au unaumia kisa kumshabikia au kumsikiliza au kumuona mgombea fulani. MIMI SINTAHUDHURIA MKUTANO WOWOTE WA KAMPENI MAANA NINAJUA SERA ZA KILA CHAMA. Mie sio LOFA WALA MPUMBUVU. Wewe Je?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments