Hili ni Suala la Tofauti Tu - Siyo Chuki
Na. M. M. Mimi Mwanakijiji
Wao wana haki ya kumtaka Lowassa kama Rais wa Tanzania; na sisi tunahaki ya kumkataa Lowassa kama Rais wa Tanzania. Wao wana haki ya kumtaka awaongoze katika kuleta mabadiliko yoyote wanayoyadhania na sisi tuna haki ya kumkataa kuleta mabadiliko yoyote tunayoyadhania atakuja nayo!
Wanaweza kabisa kusema Lowassa anafaa na kwanini kura zao zote na za familia zao zitamwendea yeye na sisi tunaweza kabisa kusema kuwa sisi na familia zetu (hata tusioweza kupiga kura sasa) tutamnyima hizo kura zetu. Wao wanaweza kusema hawajali lolote kuhusiana na historia ya Lowassa na aina ya uongozi wake na hivyo hawajali lolote litakalosemwa au linalojulikana kuhusu Lowassa na kundi lake; na sisi tuna haki ya kusema na kuonesha tunajali yote yaliyosemwa na yanayojulikana kuhusu Lowassa na aina ya uongozi wake na watu wanaomuamini.
Kumbe utaona hili siyo suala la kuburuzwa kwenda upande mmoja au mwingine ni suala la kutambua na kuonesha tofauti zetu ili watu watakapofanya ule uamuzi Oktoba 25 wawe wamefanya uamuzi baada ya kutafakari ya kutosha. Kama watu wamejipanga kwenye genge na unawakuta wote wanaruka kwa furaha kwenda huko chini inapofika zamu yako una hiari; ama na wewe uruke au ujiulize kwanza unaruka kwanini na unaenda kutua wapi! Wakikuambia wewe ruka tu kwani si na wengine wanaruka na wewe ukaruka halafu ukafika chini umevunjika kiuno huwezi kulia "mbona hamkuniambia"; kwani wanaweza kuuliza "kwanini hukuuliza"?
Au chukulia mfano mwingine mbaya kidogo; unawakuta watu wanakimbia na mioyo inawatoka kibinadamu na wewe itabidi ugeuze ukimbie, lakini ukiendelea kukimbia tu halafu huoni kinachokufukuza na wenzako bado wanakimbia ama itabidi ufike mahali ujiulize 'unakimbia nini' au uache kukimbia na usubiri kuona hicho kinachowakimbiza. Lakini ukisubiri sana ukaendelea kukimbia halafu baada ya siku nzima ya kukimbia ukauliza jamani "tunakimbia nini" na wao wakakuambia "tunafanya mazoezi ya riadha" sijui ni nani ataonekana mjinga kati yenu. Huwezi kulalamika na kusema "sasa mbona hamkuniambia mmenipotezea muda wangu kukimbia kutwa nzima"; wao watakuuliza "wewe hukutuuliza!"
Au umependa basi ambalo umekuta abiria wengi wanapanda na linaonekana ni maarufu kwelikweli; na unawaona watu wanatoka kwenye mabasi mengine wanaingia. Ukipanda basi hilo na kuimba nyimbo za "dereva wetu ongeza mwendo" na basi likaondoka kituoni na kuanza safari na wewe ukafurahia na wasafiri wenzako baada ya safari ya muda itabidi ujiulize tu "tunaenda wapi?" ukiambiwa "hatuendi popote sisi tunamfuata dereva tu anavyoendesha kuzunguka mjini" huwezi kukasirika. Utakasirika kwa lipi? Kwani walikuambia wanaenda wapi?
Wiki iliyopita kundi la wakimbizi wa Syria huko Bulgaria walijikuta wanakataa kupanda treni waliloambiwa linaenda Austria kumbe lilikuwa liwepeleke kwenye kambi za wakimbizi; wengine walishapanda lakini wale walioshtuka waligoma wengine hata kulala relini! Hawakutaka kupelekwa wasikotaka kwenda!
Kumbe, hili ni suala la tofauti kubwa na za msingi. Namheshimu kila mtu anayemtaka Lowassa, hutanisikia nikimtukana mtu au kumkejeli mtu kwani kufanya hivyo ni kukubali amekushinda kwa hoja wakati hadi hivi sasa sijaona hoja yoyote ya kwanini Lowassa awe Rais zaidi ya "tumechoka CCM". Watu waliochoka hawapaswi kufanya maamuzi mazito! Ndio maana hatuwaachi madereva, madaktari au hata mainjinia kufanya kazi au maamuzi mazito wakiwa katika hali ya uchovu, uchungu au hasira! kwani kama hawatosababisha madhara kwa watu wengine wanaweza kusababisha madhara kwao wenyewe.
Katika hali ya kuchoka ndio maana unasikia watu wanasema "hata jiwe", "Liwalo na liwe", "haijalishi wanasema nini", "Mimi Lowassa tu" n.k Baadhi ya kauli zinakufanya uamini kweli hawa ndugu zetu hawataki tena kufikiri kwani kweli kweli wamechoka!
Sisi wengine bado hatujachoka kufikiri, na hatujachoka kuelewa kiini cha matatizo yetu. Tusichokubali na tunachokikataa bila kumwomba radhi yeyote au kuona haya ni aina ya uongozi wa mtu kama Lowassa ambao tumeshauona na umeshaligharimu taifa. Ni tofauti hii ya msingi inayotufanya kumkataa pamoja na ahadi zake zote na za wale ambao wanajaribu kumlazimisha katika fikra za Watanzania

0 Comments