Msuya: Nashangaa hivi Sumaye anafikiri!
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2015, Livingstone Luhere, amefanya mahojiano na waziri mkuu msitaafu Cleopa Msuya, ambaye pamoja mambo mengine ameelezea maoni yake juu ya kuhama kwa waliokuwa mawaziri wakuu Fredrick Sumaye na Edward Lowassa kujiunga na Upinzani. Endelea..
Raia Mwema: Vyama vimekwishakuteuwa wagombea na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshazindua Ilani yake, unadhani haya yaliyomo kwenye Ilani yanaweza kuivusha Tanzania kufika inakotaka kufika?
Msuya: La kwanza na kubwa siyo malengo ambayo yameandikwa hapa, kitu cha kwanza ni uongozi, ukipata uongozi mzuri, wenye vision (maono), wenye kuelewa shida zetu na matatizo yetu na tunataka kwenda wapi, haya yanatekelezwa bila matatizo.
Lakini ukikosea kwenye uongozi hilo linakuwa tatizo, na mimi nashukuru Chama Cha Mapinduzi kimeteua timu ambayo nafikiri kwa sifa zake na uchaguzi wake, ni watu wasio na madoa madoa, ni watu waadilifu, ni watu wachapakazi, ni watu ambao hizi tuhuma za umma kwamba tungeweka mafisadi na walaji wa mali ya umma, hawa hawana tatizo hilo.
Na sasa tunachoomba ni Watanzania wawape kura na hii timu ya Magufuli na Mama Suluhu waanze kujenga uongozi utakaotuongoza kwa miaka mitano ijayo, wenye watu wenye kufanana nao na kuondoa yale madoa madoa ya watu wenye matatizo, wapo ndani ya serikali na ndani ya chama maana wako wengi hawa katika taifa letu. Ili kama ni boti iweze kwenda vizuri. Wajenge momentum na kusafisha uogozi ambao utatuvusha kwa miaka mitano ijayo. Hayo ndiyo matumaini yangu. Sasa wananchi wawape kura na wakiingia wajenge timu ya wasaidizi kuanzia kwenye Baraza la Mawaziri, serikali, mikoani na kwenye chama, ambao wataogoza katika njia hii, kama vile chama kilivyowateuwa watekeleze malengo hayohayo.
Raia Mwema: Kabla ya uteuzi wa wagombea kwa vyama, ulisema mafisadi wakitoka watatoka na mafisadi wenzao….
Msuya: Si unaona wametoka. Si wamekimbia. Tusubiri kule wanakokwenda. Taifa litaanza sasa kujua nani anatufaa na nani hatufai. Na ndiyo woga niliokuwa nao. Tungeendelea kubaki na wale ndani CCM ingepata matatizo. Ni bora
wametoka.
Raia Mwema: Ina maana wewe hutishiki kuondoka kwa Lowassa na Sumaye?
Msuya: Sitishiki hata kidogo. Tumejisafisha. Maana yake si mtu anajisafisha mwenyewe? Anaamua, na wengine hawa hata unashindwa kujua wanataka nini?
Kwa mfano, kuna mwenzetu amekuwa waziri mkuu kwa miaka 10. Alitamka mapema kwamba yeye kama kiongozi mmojawapo akichaguliwa ataondoka. Sasa amehama na amemfuata huko. Ndiyo unashangaa hawa watu wanafikiri au nini.
Lakini hilo si tatizo. Suala ni kwamba umeachiwa chama na wale waliokuwa wana mashaka mashaka wameamua kuhama acha wahame.
Raia Mwema: Mawaziri wakuu wastaafu hamna klabu ya kukutana kuzungumza?
Msuya: Tatizo si klabu. Tatizo katika mambo haya sisi ni sehemu ya senior citizens, tuko na uzoefu kiasi fulani. Tuliona mambo ndani na saa tunaona tukiwa nje. Kwa lugha nyepesi wanasema ni fahari ambayo watu wanaweza kuichota. Tutaendelea kutoa ushauri kila tunapoona kama ambavyo watu wanahitaji.
Raia Mwema: Hili la mtu kutoka CCM na kwenda Upinzani aliyekuwa na ngazi ya juu kama waziri mkuu, unalitazamaje?
Msuya: Mimi nimestaafua lakini nimesema nitabaki muumini wa CCM kwa sababu kifalsafa, kimtazamo naamini sera za CCM na iko imara. Kunaweza kuwa na matatizo ya hapa na pale katika utekelezaji, lakini haya ni matatizo ya kibinadamu.
Lakini kusema nataka nitoke, nitoke niende wapi? Sasa hao waliotoka ndiyo watawaambia kilichowatoa nini, maana mpaka leo mimi sioni hoja ya kusema anatoka anakwenda wapi?
Raia Mwema: Wanasema ni kutokana na mizengwe kwenye uteuzi wa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi.
Msuya: Tunaweza kubishana kwa maneno. Unajua uchu wa madaraka ni tatizo. Ukiwa na watu 42 au 38 na nafasi inayotafutwa ni moja, lazima kuna watu wataachwa.
Hata kama ni mpira mnajua kwamba mnakwenda wengi lakini mnajua ni mmoja tu atashinda, sasa akishinda huyo ndiyo muanze kusema mizengwe. Hakuna hoja hapo. Ni kwamba mchakato ule wa kutafuta haukukuchagua wewe basi. Lazima ulikubali hilo.
Na ndiyo maana ya demokrasia, inataka wengi mnajitosa lakini atakayeshinda ni mmoja au wachache, basi hiyo ni uwe mfumo wa Kimarekani au Uingereza, kokote kule.
Sasa kuna watu wanalalamika, sijui 'system' inafanya nini, mimi sielewi. Kwa maoni yangu, huku ni kukuza mambo kusikokuwa na msingi.
Raia Mwema: Nini nasaha zako kwa vijana wanaoibukia kwenye siasa?
Msuya: Vijana sasa tuwaachie wenyewe wajifunze. Maana watatusoma wote, tunaobaki na wanaoyumba yumba. Watafikia hitimisho kwamba wanatafuta mtu wa aina gani.
Mimi ninaamini katika haya yaliyofanyika katika nchi yetu kwa miaka hii 50 iliyopita na naamini huu uongozi ulioteuliwa na CCM wa Magufuli na mama Suluhu na sifa zao, ni ishara kwamba tutaendelea na mtazamo wa Tanzania wa kazi, kuhudumia watu, kupambana na maradhi mengi na ujinga.
Raia Mwema: Unaweza ukasemaje kwa hatua walizochukua Dk. Wilbrod Slaa na Profesa Ibrahim Lipumba kuachia vyama walivyokuwa wakisimamia?
Msuya: Hawajatamka waziwazi ni nini kilichowatoa. Lakini kwa upande mmoja kama yanayosemekana ndivyo, kwamba wanapinga watu wenye sifa mbaya kujiunga na vyama vyao, mimi nawaunga mkono.
Mtu hawezi kusafishika kwa sababu leo alikuwa na sura mbaya hapa na ulimsema hivyo halafu ahamie kule wamkumbatie. Ni vitu ambavyo havieleweki.
Ndiyo maana nasema hivi vyama vinavyounda Ukawa sina imani nao kwa sababu, kama walikuwa wanashutumu baadhi ya watu waliohamia humo mwao, haiwezekani ghafla tu wakawa ni lulu. Kama kuelewa kwetu ndiyo hivyo sasa inakuja sababu kwanini wamewapokea, sasa tunauachia umma wenyewe uamue.
Raia Mwema: Wakati wa mchakato wa uchaguzi huu kwa vyama karibu vyote tumeshuhudia matumizi ya fedha kwa njia isiyo halali, kinyume na misingi ya demokrasia, unadhani tatizo ni nini na nini kifanyike?
Msuya: Mimi sidhani kama tatizo letu ni kanuni. Watu wanajua kitu wanachotafuta. Watu wanajua jinsi ya kupata viongozi wazuri, na kama ni viongozi wafanyeje kazi vizuri, na taratibu zinaeleweka kidemokrasia.
Tatizo linakuja mahali wanapotaka kukunja kunja hizo taratibu. Kama huwezi kumshawishi mtu kwa kumweleza sera zako unatumia fedha ili akuchague, kama unafikiri wau wanashida na ajira na usafiri na kipato unawapa shilingi ili wakukimbilie, hilo siyo jawabu la tatizo.
Jawabu la tatizo ni kuweka msingi utakaoweza kuondoa kiini cha huo umasikini. Kwa hiyo, shida tuliyo nayo ni watu wanataka kutumia matatizo ya watu kufikia malengo yao ya kutafuta madaraka.
Raia Mwema: Mara ya mwisho tulipofanya mahojiano, wakati unazungumzia vyama vingi, ulisema vinatakiwa kuwa na uongozi imara na vijiainishe, unadhani kuunda Ukawa, wamefanikiwa katika hilo?
Msuya: Tunazungumza kitu kinaitwa Ukawa, ni nini, hiki ni kama kivulivuli tu hivi. Kisheria hakuna kitu kama Ukawa. Kuna vyama ambavyo vimesema vitashirikiana.
Sisi wengine tulioko nje tulisema, kama kweli hawa watu wameamua kushirikiana kwanini wasivunje vyama vyao wakaunda chama kimoja? Wasiwe ni CUF, wasiwe NCCR –Mageuzi, wasiwe Chadema. Waunde kitu ambacho kinaeleweka kina sera, kina uongozi na kina lengo.
Lakini kukusanya tu watu for convinience tu hivihivi, halafu hujui ni nini, tutafanya makosa kusema tunapigia Ukawa, hakuna kitu kama hicho.
Na ndiyo sababu Lowassa amehamia kule lakini amekwenda Chadema. Inasemekana kuwa Sumaye ingawa amekwenda huko atajiunga NCCR – Mageuzi.
Hawawezi kwenda Ukawa kwa sababu hakuna kitu kama hicho kisheria. Na hawezi kutoa ilani kwa sababu inatolewa na chama, itakuwa ya Chadema, au CUF lakini Ukawa hawawezi kuwa na Ilani.
Raia Mwema: CCM wametoa Ilani ikiwa na vipaumbele vingi, wewe ungekuwa unamshauri Rais ungemuasa aanze na vipaumbele vipi?
Msuya: Kwa sasa hivi kitu ambacho kimenipa matumaini ni kwamba katika yote haya taifa lilihitaji leadership (uongozi) ambao ni mzuri, yenye dalili za kuwa imara, na kupendwa na wananchi ambayo itatuvusha. Ile leadership iko kwenye hii timu ya Magufuli na mama Samia Suluhu.
Imani yangu ni kwamba Watanzania tukiwapa kura, wataanza kujenga watu wenye mitazamo inayofanana nao, ili iwasaidie kutengeneza hayo yote yaliyowekwa kwenye ilani. Bila hiyo kuzungumza hivi vitu vingine ni hovyo tu kwa sababu, kitu hiki lazima kiwe na umiliki wa mtu ambaye atasema tutakitekeleza.
Sasa timu hii wakifanikiwa watajenga timu ambayo itatupeleka vizuri. Sasa katika safari hiyo, haya yote yaliyotajwa ni muhimu lakini yako yale mengine yenye ubora zaidi.
La kwanza kwa sababu uongozi unafanya kazi ya usimamizi wa shughuli za serikali uwe mzuri na kwa ufanisi, lakini pili uzalishaji ambao ndiyo unatengeneza uwezo wa kifedha na kiuchumi kuwezesha mambo yaende.
Lazima misingi ya uzalishaji mali ijengwe ili uchumi uweze kuendelea, katika mchakato huo wa uchumi kukua kuna maeneo ambayo yamechelewa kukua ambayo yanatakiwa yaboreshwe kwa mfano, usafiri wa reli, bandari, anga, umeme.
Reli iimarishwe tusitegemee barabara tu. Kwa nchi kubwa kama yetu huwezi kutegemea barabara tu kusafirisha mizigo yote. Ndiyo maana barabara zetu zinaharibika. Kwa usafiri wa anga, ni lazima uchumi unavyokuwa ukue haraka haraka, kwa mfano, kutoka hapa kwenda Sumbawanga, ukichukua gari unaweza kutumia siku nzima au mbili lakini kwa ndege unakwenda haraka.
Raia Mwema: Kuna neema inakuja, mwezi ujao gesi inaanza kutumika, hii imekuwa changamoto kwa nchi nyingi, kwa maoni yako unashauri itumikeje?
Msuya: Kwanza ni vizuri Watanzania tusije tukatumbukia kwenye shimo la kutazamia miujiza kutoka kwenye hii rasilimali ya gesi.
Hii rasilimali ndiyo tumeambiwa ipo. Lakini mpaka itoke, ianze kutumika na kuleta matokeo kwa wananchi itachukua miaka mingi.
Kwa sasa hivi mipango ilivyo wanaitumia hiyo gesi kuzalisha umeme. Hiyo ni upande mmoja na itarahisisha mambo, lakini hatma ya hiyo gesi kama iko nyingi, itatakiwa isaidie kwenye viwanda kuzalisha bidhaa nyingine tuweze kuwa na kitu cha kuuza nje. Tupate pesa za kigeni ili tufanyie mambo mengine kama kujenga reli, kuimarisha huduma za afya, elimu na mambo mengine mengi.
Raia Mwema: Kampeni ndiyo hizo zimeanza, una wito gani kwa Watanzania?
Msuya: Kwanza Watanzania mimi nina imani nao, ni watu wazuri, tumekaa miaka 50. Historia yao inaonyesha kwamba ni watu wanaoweza kuaminika kuchagua viongozi wazuri.
Pili, wachague viongozi ambao watatutumikia vizuri bila hila bila ujanja, bila njia ya kujinufaisha wao wenyewe. Na timu hii iliyoteuliwa na CCM nafikiri ina kila sura ya kwamba wakifanikiwa wataweza kufanya kazi vizuri. Tunaomba Watanzania wawachague wawafanyie kazi, tundokane na haya matatizo ambayo siku za karibuni baadhi ya watu wamekuwa wakijificha kwenye mifumo wanakuwa mchwa mchwa wa mali za umma.
Watu wakapige kura, katika taifa letu mimi nimejifunza, katika nchi zilizokomaa wakubali kwamba kuna taasisi fulani za kidola zitabaki za kidola bila kujali chama gani kinatawala. Polisi ni mojawawapo, Jeshi na Mahakama pia.
Kwa hiyo juhudi za watu kusema Jeshi ni CCM, ni kutumia lugha vibaya, na kuweka mazingira mabaya, lazima vyombo kama Jeshi na Polisi vilindwe na vyama vyote vya siasa, kwa sababu ni vyombo ambavyo vitatuongoza huko mbele ya safari.
Ukivivuruga hivyo ukaanza kuvipaka matope, baadaye utakosa msingi wa kusimamia, na hivi vinatumia sheria, kanuni zilizotungwa na Bunge, vifanye visiwe vinayumbishwa na chama chochote, na vyama vya siasa lazima viheshimu huo msingi. Tukiuvuruga huo huko tunakokwenda tutakuwa na matatizo.
Raia Mwema
Toleo la 421,2 Sep 2015

0 Comments