[wanabidii] Mbatia na Ukawa uzushi na uongo dhidi ya rais Kikwete haviwezi kumpeleka ikulu Lowassa

Sunday, September 27, 2015
By mkulimawakiteto View Post

Kadri siku za kufanya uchaguzi mkuu unavyokaribia ndivyo tunavyowajua wanasiasa wetu na kuwato maana kwa kuwa wamekuwa wakionyesha uhalisia wao kwa kushindwa kuficha asilia na hulka zao kwa jinsi walivyo akiwemo Mwenyekiti wa Nccr Mageuzi Jemsi Mbatia.

Mbatia amekuwa mzushi na Muongo katika harakati zake na Ukawa ili kuwaghiribu watanzania wafanikishe kumpeleka ikulu Edward Lowassa kwa njia yeyote ile hata kama ni kwa kusema uongo ili mradi tu mgombea wao ashinde uchaguzi mkuu bila kuangalia athari za maneno yao ya uongo wanayojaribu kuyapandikiza vichwani mwa watanzania.


Nilikuwa namchukulia Mbatia kama mwanasiasa mkweli na Mweledi na makini lakini nimekuja kujua kuwa hayupo hivyo kama tulivyokuwa tukidhani watanzania wengi, Mbatia amekuwa kama wanasiasa wengine wachumia tumbo ambao wamekuwa wakipoteza heshima zao kila kukicha.

Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari Jemsi Mbatia alidai kuwa ktika kipindi cha miaka 10 chenye wastani wa siku 3,650 Rais Kikwete amesafiri mara 409 na alikuwa akikaa nje ya Tanzania kwa wastani wa siku tano katika kila safari hivyo jumla yake kuwa 2,045.

Mbatia akijumuisha salafri hizo za rais Kikwete alisema jumla ya asilimia 56 ya muda wake aliokaa madarakani hadi kufikia sasa, Mbatia alifika mabali zaidi kwa kusema uongo kwa kusema hgarama ambazo taifa imezibeba kutokna na safari hizo kwa mujibu wa safari hizo ni trilioni 4.5.

Serikali iliingilia kati uzushi huo na Mbatia na kueleza uhalisia wake. Wizara ya mambo ya nje na ushirikino wa kimataifa ilitoa ufafanuzi kuwa tangu rais Jakaya Kikwete aiingia madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa viongozi wakuu rais, makamu wa rais na waziri mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa mwaka 2014/2015. Kwa ajili ya idara ya itifaki.

Kwa miaka mingine yote imekuwa wastani kati ya bilioni 5 mpaka 25 kulingana na mahitaji ya idara husika ilisema taarifa hiyo ya wizara ya mamabo ya nje.

Hebu Tuangalie baadhi ya mafanikio ya safari za rais kikwete tangu aingie madarakani, Inawezekana kuwa rais Kikwete ndiye kuwa ndiye anayeongoza mara kwa mara kwa safari za kwenda Marekani kuliko tawala zote tatu zilizopita.

Katika ziara hizo za Marekani za rais Kikwete, wakati wa utawala wa George Bush ulisaidia misaada ya kupambana na maralia dawa na chanjo na vyandarua.

Halikadhalika tulipatiwa msaada wa dola za kimarekani million 700 kupitia mfuko wa milleniam challenge (MCC) fedha ambazo zimesaidia ujenzi wa barabara za Mtwara-Masasi-Tunduru Songea hadi Mbamba Bay na ile ya Rukwa hadi Sumbawanga.

Pia rais alifanya ziara katika nchi za Brazil na India ambapo katika ziara yake ya nchini India ilizaa mradi mkubwa wa kuboresha miundombinu ya maji ndani jiji la Dar es Salaam pamoja na ujenzi wa chanzo kipya cha maji cha katika mto Ruvu, Bagamoyo.

Ziara za rais Kikwete nchini nBrazil ndizo zilizoiwezesha Tanzania Kupata wataalam wa mahiri katika utafiti wa gesi na miradi iliyozaa ujenzi wa visima vya gesi katikika mkoa ya Mtwara uliopeleka umeme wa uhakika kwa wana Mtwara.

Safari za rais Kikwete nchini Korea zilileta matunda ya ujenzi wa mto Magarasi ambapo ujenzi wa mto huo umeufungua mkoa wa kigoma ambao ulikuwa nyuma kimaendeleleo. Kigoma imefunguka kwa shughuli zote za kiuchumi ikiwemo utalii ambazo zitaboresha maisha ya wana Kigoma.


Hali kadhalika Ziara za rais Kikwete nchini China ilipelekea kuzaa ziara kubwa ya rais Xi Jinping wa china ambayo ilikuwa ziara yake ya kwanza barani Afrika. Katika ziara ya Xi wa china tulishuhudia Tanzania ikiingia mikataba mikubwa 17 ya miradi mbalimbali ya kimendeleo isiyokuwa na hata chembe ya masharti wala hasara kwa Taifa.

Baadhi ya mikataba hiyo ni pamoja na ujenzi wa bandari ya bagamoyo itakayokuwa bandari kubwa kuliko zote ukanda wa jangwa la Sahara la Afrika. Ujenzi wa viwanda vya aina mbali mbali ambapo ujenzi wote huo utaongeza ajira nchini.

Pia kulisainiwa mkataba wa ushirikiano wa kitaaluma utakaowawezesha maelfu ya watanzania kupata ufadhili wa kusoma fani mbalimbali katika vyuo vikuu nchini China kwa kufanya hivyo adui ujinga tutazidi kumthibiti.

Rais Kikwete amefanya juhudi kubwa za kutangaza vivutio vya Utalii Nchini akiwa nje katika zira zake ambazop zimewasidi kuongeza idadi ya watalii na safari za, Mashirika ya Ndege ya Qatar Airways, Fly Dubai na Turkish Airlines kuongeza idadi ya safari zao nchini Tanzania. Juhudi hizo zimesaidia kuwashawishi watalii wengi zaidi kuitembelea Tanzania.

Idadiya watalii wa nje imeongezeka kutoka 1,095,884 mwaka 2013 hadi watalii 1,102,026 mwaka 2014/2015. Mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 1,853 mwaka 2013 hadi Dola za Marekani 1,983 mwaka 2014, sawa na ongezeko la asilimia saba (7). Yote hayo kutokana na zira za rais Kikwete Nje ya Tanzania.


Mbatia anapaswa anapoeleza hasara za Safari na gharama zake pia awe anaeleza faida ya safari hizo lakini asipofanya hivyo atakuwa sawa na wanasiasa wengine wachumia tumbo ambao huwapotea haraka katika tasnia nzima ya siasa hapa nchini.

Pia namalizi kwa kusema Tunajua kuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi ni vizuri Mbatia na wenzake wakatangaza ilani yao kuwa nini Watawafanyia Watanzania badala ya kueneza uongo ambao huwa haudumu hata siku moja kwa kuwa hautachuwa muda mrefu kugundulika na muenezaji wa uongo huo kuishia kudharauliwa.

Namuhusia Mbatia badala ya kutumia muda mwingi kuzua mambo ya uongo ni bora akatumia muda huo kueleza na kunadi sera na ilani ya ukawa na kumsafisha mgombea wo Edward Lowassa na kashfa mbalimbali za kifisadi zinazomundama.

0789976314

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments