Hii ni kutoka kwenye mahojiano kati ya
Deus Bugaywa, Mwandishi wa habari mkongwe, na mwanaharakati, Mama Ananilea Nkya kama yalivyochapishwa kwenye gazeti la Raia Tanzania, makala ya tarehe 3, April, 2015.
Nimechukua swali moja tu la mwisho na majibu yake kama lilivyo kutoka makala iliyopewa jina "Wapiga kura kama fungu dogo la dagaa"
....huenda uchaguzi wa Oktoba mwaka huu ukatoa fursa pana zaidi kwa wafanya biashara ya madawa ya kulevya, majangili na wakwapuaji wa mali ya umma kununua uongozi...
Raia Tanzania; Unazungumziaje nafasi ya upinzani katika uchaguzi ujao, ukizingitia kujiunga kwa Zitto na ACT?
Ananilea: Itategemea tuendako nguvu ya fedha itafanikiwa kumnunua nani na itashindwa kumnunua nani katika vyama vya upinzani maana ninaamini siyo kila anayeingia kwenye siasa anafanya hivyo kwa sababu ana uchungu na maisha ya Watanzania walio wengi. Ninaamini kuwa wako baadhi wameingia au kuingizwa kwenye siasa ili nchi yetu iendelee kuwa na siasa ambazo kikundi cha wachache kitanufaika kwa kukamata dola hata kama kwa kufanya hivyo wananchi wengi wataendelea kuteseka kwa ufukara kipindi kirefu kijacho. Hivyo sisi wananchi tunasubiri tuone, hatua hiyo ni mpango wa kudhoofisha upinzani ili bunge lijalo liwe dhaifu zaidi au ni mpango wa kuharakisha ukombozi wa wengi kwa kuimarisha sauti ya wananchi katika vyombo vya maamuzi baada ya uchaguzi ujao.
Swali langu: Kwa kauli hii (nimeikariri hapo kwenye jibu lako):
..Itategemea tuendako nguvu ya fedha itafanikiwa kumnunua nani na itashindwa kumnunua nani katika vyama vya upinzani maana ninaamini siyo kila anayeingia kwenye siasa anafanya hivyo kwa sababu ana uchungu na maisha ya Watanzania walio wengi. Ninaamini kuwa wako baadhi wameingia au kuingizwa kwenye siasa ili nchi yetu iendelee kuwa na siasa ambazo kikundi cha wachache kitanufaika kwa kukamata dola hata kama kwa kufanya hivyo wananchi wengi wataendelea kuteseka kwa ufukara kipindi kirefu kijacho...
1. Jibu hili lilimaanisha nini ukizingatia uliulizwa kuhusu ujio wa Zitto ACT?
2. Bado kauli hii iko valid? Kama ungeulizwa hili swali leo ungetoa jibu hili hili au au una majibu tofauti, hasa kwenye suala la nguvu ya fedha kuununua upinzani?
3.Ulimaanisha nini kuhusu watu baadhi kuingizwa au kuingia kwenye siasa ili kujenga kikundi cha watu fulani kukamata dola, ukizingtia tumeona hadi viongozi wa kiroho wakiingia kwa kasi kwenye siasa za nchi hivi karibuni?
4. Unaweza kufafanunua ulimaanisha nini kuhusu kujiunga kwa Zitto ACT kuwa "hatua hiyo ni mpango wa kudhoofisha upinzani ili bunge lijalo liwe dhaifu zaidi au ni mpango wa kuharakisha ukombozi wa wengi kwa kuimarisha sauti ya wananchi katika vyombo vya maamuzi baada ya uchaguzi ujao" (JIBU HILI NI TATA,-umekubali, umekataa au uko neutral?)
Ni hayo tu.
Omukunirwa Ireneus.
Makala hii iko online kwenye anwani hii:
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en ---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to
mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to
mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit
https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAN5khk558FczebAv0MaZZxqv5-%3Dho6D-mU3S1AHPZZFTsaU2iQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
Share this :
0 Comments