[Mabadiliko] Neno La Leo: Udini Ni Karata Ya Hatari..

Tuesday, September 08, 2015


Ndugu zangu, 

Kwa mnaonifuatilia mtakumbuka, kuwa kwenye Neno langu fupi la usiku la January 5, 2014 niliandika; 

"Katika Tunayoyapitia, Chonde Tusiitumie Karata Ya Udini...
Ndugu zangu,
Nchi yetu inapita katika kipindi kigumu sana kupata kutokea tangu tupate uhuru. Kuna namna njema ya kusonga mbele. Ni endapo tutatanguliza busara na hekima.
Na chonde, katika yote haya tunayopitia, tusitumie karata ya udini kufanikisha malengo binafsi, ya makundi na hata vyama vya siasa. Ni karata ya hatari sana.
Kuna tuliokwishaanza kuziona ishara......
Maggid Mjengwa,
Iringa." ( Neno Fupi La Usiku, Januari 4, 2014)

Ndugu zangu,

Nimeshtushwa sana na video iliyosambaa ikimwonyesha mmoja wa wagombea urais akitumia karata ya udini kuomba kuchaguliwa. Kama ni video ya kweli, basi,jambo hili halifai kabisa. Tulikemee vikali. Haliendani na misingi ya uwepo wa taifa letu. Hii ni nchi yetu sote. Ni nchi ya wote. Rais atakayechaguliwa atakuwa ni Rais wa wote, si wa Wakatoliki, Walutheli, Waislamu na wengineo. Ni rais wa Watanzania.

Ni imani yetu, kuwa aliyetoa kauli hiyo ni mwanadamu, na ulimi hauna mfupa. Kwamba haraka atarekebisha kauli yake hiyo. Vinginevyo, kwa kuchelewa sana, hata wapinzani wake wa kisiasa, ni kama amewapigia penalti mikononi. Tunaona sasa wakiitumia kikamilifu kauli hiyo yenye kuwakera Watanzania kama mtaji wa kisiasa.

Maana, Watanzania wanajua, kuwa kamba hukatikia pabovu, na palipo na ubovu kwenye kamba inayowaunganisha Watanzania ni kwenye tofauti za kidini kama zikitumiwa kuwatenganisha. Yaweza kuhatarisha amani ya nchi.

Nchi yetu imedumu kwa miaka 54 sasa ikiwa ya amani na utulivu kutokana na misingi imara ya ujenzi wa Umoja wa Kitaifa tuliojengewa na waasisi wa nchi hii. Misingi iliyohakikisha kunakuwepo na Umoja Na Amani. Hizo ni silaha zetu mbili muhimu kama taifa.

Ndani ya miaka 54 ya Umoja Na Amani tumeshuhudia sio tu nchi jirani zikiingia kwenye machafuko na watu kuuana, bali hata nchi za Ulaya zikiingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mfano wa machafuko ya nchi za Balkan. Tanzania kama nchi tumebaki salama. Kamwe tusikubali kuweka rehani Umoja Na Amani ya nchi yetu.

Na tuendelee na ushindani wa kisiasa kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Tuendelee kutofautiana na kubishana kisiasa.
LAKINI, tuepuke siasa za kibaguzi, iwe wa rangi, kabila, au kanda. Na chonde chonde, tusitumie karata ya udini katika kufanikisha ushindi kwenye ushindani wa kisiasa.

Ni Neno La Leo.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Maggid, 
Iringa.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye4SLmOD5D_C1-0eXv2hPgKSaBOPKZna8F57N4iCH_EfxA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments