Fw: [wanabidii] MAJIBU KWA MWINGILU NCHEMBA

Tuesday, September 15, 2015
Aksante mama kwa kutusaidia kuueleza umma wa watanzania kinachotakiwa kufanywa kwa sasa kama kweli wagombea wetu wako serious katika kuondosha umasikini katika jamii yetu au ni maslahi binafsi

On Tuesday, 15 September 2015, 12:02, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Nakushukuru  kiongozi wangu wa kitaifa  Mwingilu Nchemba kwa vile  umekuwa ukisoma hoja zangu humu kuhusu CCM kumpakazia Edward Lowassa  ufisadi wa Richmond ili serikali ya CCM isionekane machoni  umma kwamba ndiyo inaendekeza na kunufaika na ufisadi na rushwa.

Hata hivyo  wananchi wengi sasa  wanafahamu kuwa  chanzo cha  ufisadi na rushwa nchini ni mfumo wa utawala wa serikali ya CCM  uliowekwa kimkakati kuwezesha ufisadi na rushwa kwenye fedha na rasilimali za taifa hili kwa lengo la CCM kubaki madarakani kunufaisha watawala wachache na wawekezaji kutoka nje (wakoloni wa kisasa)huku mfumo huo ukizalisha mamilioni ya Watanzania maskini wa kutisha.

Hakika nilitegemea kuwa hoja zangu za kimaendeleo ninazoziandika humo zingekuwa zimekusaidia kupata uelewa kama vile ambavyo zimemsaidia mgombea Urais wa CCM Dr John Magufuli kutambua kuwa hali ya maisha ya Watanzania wengi ni mbaya na wanataka mabadiliko ya uongozi wa nchi yao.
Badala yake naona unaendekeza u-CCM zaidi kama vile Tanzania ni mali ya CCM na siyo mali ya Watanzania wote.

Ulipokuwa unatafuta Urais ulikuwa unatumia lugha ambayo baadhi yetu tulidhani umeelewa kuwa wananchi wanataka mabadiliko.
Kumbe bado. Hakika  kama  maandishi haya hapa umeandika wewe, tena ukiwa Naibu  Waziri wa fedha (mlinzi wa fedha za Watanzania), basi zile maski baadhi yetu tulizokuwa tumekupa za Urais asilimia 55, tunalazimika kupunguza hapo asilimia 20.

Tumezipunguza maski hizo  kwa sababu inaelekea hujaelewa kwamba Watanzania wanataka mabadiliko--mabadiliko ya kuweka msingi wa Kikatiba (Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi) ili  kuondoa mfumo unaozalisha kikundi kidogo cha watawala matajiri wa kukufuru na mafuriko ya wananchi masikini wa kutisha.

Nakutakia kampeni njema nikiamini kwamba  kwenye kampeni zako utaweka maslahi ya  Watanzania na Tanzania kwanza kama kweli unaitakia  nchi yetu amani, utulivu na maendeleo ya kunufaisha wananchi wote na watawala wachache. Mungu ibariki Tanzania.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments