[wanabidii] LIPUMBA; UMECHELEWA JAPO SIO SANA

Wednesday, August 05, 2015
Jumapili iliyopita katika kipindi cha watoto ITV Shangazi alikuwa anawasimulia watoto kisa cha wanyama kumtafuta mfalme. Ili kutochosha namalizia mwaishoni wakati simba anachaguliwa kuwa mfalme. Kamati ya uteuzi ilimchagua simba atawale baada ya 'kuomba' ateuliwe yeye, kwa sababu tu wanyama wengine wangemkataliaje simba ambaye licha ya kutoogopa lakini mnyama yeyote yuko hatarini wakati wa shida na wakati wa raha?

Mimi nilikuwa nayashangaa mambo yanayoendelea ndani ya UKAWA na sababu ya UKAWA 'kuitaka' CHADEMA imtoe mgombea urais. Lakini CHADEMA 'inayoombwa' kutoa mgombea urais 'haina' mtu anayeweza kuwa rais. Inamendea atakayetemwa na CCM. Ona sasa. CHADEMA inaye kijana machachali ambaye angeweza kuwa mgombea mwenza. Mr. Mwalimu. Badala yake inamchukua mtu muhimu na anayependwa sana CUF anakuwa mgombea mwenza. 'Huyu mfalme' anayeazima wa kukikalia kiti cha ufalme kwa nini asiwaachie wenye uwezo wakawa wafalme?
Nalisema sasa ili wasipochukua tahadhali likitokea watakaokumbuka wajifunze. CHADEMA yaweza kuwa na siri ya kuivunja CUF. CHADEMA haikubaliki Zanzibar. Kijana wake machachali Mwalimu anaandaliwa kuwa kiongozi kwa upande wa Zanzibar siku zijazo. Kama CUF itaendelea kuwa na nguvu bado huyu kijana hawezi kukubalika Zanzibar. Umachachali wake si kukubalika kwake hasa kama bado CUF ina nguvu. Njia pekee ni kuivunja uti wa mgongo CUF. Akichukuliwa Duni akawa mwanachama wa CHADEMA atawavuta wengi kuikubali CHADEMA. Ikitokea CHADEMA ikashinda makubaliano yao waliyokubaliana bedirumu huwezi kuyaleta sebureni. Rais ataunda serikali CHADEMA inavyotaka na UKAWA itabaki historia. Uwezekano wa Duni kujiondoa na kuuacha uhondo wa umakamu wa Rais ni mdogo sana. Ikiwa hivyo basi wafuasi wa CUF watajipanga nyuma ya Duni na hivyo nyuma ya CHADEMA. Hapo CUF itabaki kwenye kumbukumbu za msajili wa vyama vya siasa.
Inahitaji kuwa na miwani mikali kuliona hilo. Na Lipumba ameliona. Ni msataarabu wa kutosha kutofanya vurugu. Tunaomkumbuka Thomas Sankara tunakumbuka. Alipogundua mkuu wa majeshi anataka kumpingua alimwita akamwambia: 'Najua unachotaka kufanya. Nikikuua sasa wataniita muuaji. Sitaki. Endelea kukifanya sina la kufanya'. Baada ua wiki moja hivi Sankara alipinduliwa na kuuawa. Mpaka leo sijawahi kumtambua Kompaure japo sina serikali ya kumuumiza kwa kutomtambua.

Nasikia Ibrahimu Haruna Lipumba anataka kuachana na siasa. Lazima akifanya hivyo atatwambia sababu. Kwa ustaarabu wake hawezi kuitaja hii. Baada ya muda tutagundua kuwa hii ninayoiandika humu leo ndiyo iliyomfanya aachane na siasa. Mnajua Lipumba ni msataarabu sana? UKAWA hoyeeee!
Nasikia mtu wa kwanza kusema dunia ni mviringo aliuawa kwa amri ya uongozi fulani. naomba nisiuawe kwanza

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments