[wanabidii] LAWRENCE MASHA KORTINI KWA LUGHA CHAFU

Tuesday, August 25, 2015
LAWRENCE MASHA KORTINI KWA LUGHA CHAFU

* ATUPWA GEREZANI

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na sasa ni Kada Mpya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Lawrence Masha amefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Leo akikabiliwa na kosa Moja tu la kutoa chafu maofisa wa Jeshi la Polisi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, Wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi alidai Kuwa Kesi hiyo ya jinai Na.190 ya Mwaka huu, mshitakiwa ametenda kosa Hilo la kutoa lugha chafu kinyume cha Kifungu cha 89(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.

Wakili Kishenyi alidai Kuwa Agosti 24 Mwaka huu, ndani ya Kituo Cha Polisi Oysterbay Jijini Dar Es Salaam, Masha ambaye ni Wakili kitaaluma alitumia lugha chafu dhidi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Juma Mashaka na maofisa wenzake wa Polisi kwa Kuonyesha Kuwa Juma na maofisa wenzake wa Polisi Kuwa ni ' washenzi na waonevu hawana shukrani,huruma wala dini maneno ambayo yalikuwa yanataka kuatarisha Amani.

Hata hivyo Masha alikanusha kosa Hilo na Hakimu Lema alisema ili mshitakiwa Huyo apate dhamana ni lazima awe na wadhamini Wawili watakao saini bondi ya sh.milioni Moja.

Baada ya Hakimu Huyo kutoa Masharti hayo upande wa jamhuri uliomba muda utahaki barua za wadhamini na muda ulikuwa umeishakwenda hivyo Hakimu Lema akaairisha Kesi hiyo hadi Septemba 8 Mwaka huu,kwaajili ya kutajwa na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani kwasababu Masharti ya dhamana bado hayajatimizwa.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com

0716 774494


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments