Inasikitisha sana kuona chama kilichokuwa na sifa hapa nchini kupinga vita ufisadi na rushwa, ndio kinakuwa chama kikuu cha kupokea mafisadi ya kila namna.
Inasikitisha sana hasa ikizingatiwa kuwa Mafisadi haya yanajiunga na chama hiki baada ya kukatwa kutoka CCM. Mtu kama Lowassa, ameondoka CCM sababu ya kukatwa na sio ameondoka kwa kupiga vita rushwa na ufisadi. Lowassa hana mapenzi ya dhati na CHADEMA.
Lowassa ni kama mtu anayeshika mwamvuli wakati mvua inanyesha, ili asilowane maji. Lowassa amenyeshewa mvua CCM kakimbilia mwamvuli ambao ni CHADEMA.
Hakika kwa hili CHADEMA wamepoteza mwelekeo kabisa, ni kama mbwa anapoamua kula matapishi yake mwenyewe! Kwa hili wamewakatisha tamaa Watanzania waliokuwa wanawaamini kuwa wapo kwa ajili ya kupambana na rushwa na ufisadi na sio kuwakumbatia mafisadi. CHADEMA walipaswa kuwa makini sana na maamuzi yao. Mimi binafsi simlaumu Lowassa kwenda CHADEMA bali nawalaumu sana CHADEMA kukosa msimamo dhabiti.
Lowassa ameingia CHADEMA ili kujaribu kutimiza ndoto zake binafsi za kuingia Ikulu na sio eti ana mapenzi na CHADEMA. Lowassa ana uchu wa madaraka, na sababu ameyakosa CCM sasa anajaribu kama atayapata CHADEMA. Mtu kama huyu ni hatari sana, na viongozi wa CHADEMA walipaswa kulibaini hili mapema sana.
Binafsi naamini kabisa ndani ya CHADEMA wapo watu wenye upeo wa kufikiri na kuchambua mambo, ambao tayari wameshahoji hili swala na watachukua maamuzi sahihi kabisa, hata kama hawataondoka CHADEMA lakini kura zao hawatampa Lowassa siku ikifika.
Mtu ambaye hawezi kuzisimamia kauli zake mwenyewe, kamwe hataweza kusimamia matakwa ya watu wengine pia. Lowassa ameonyesha dhahiri kabisa kuwa ni mtu mwenye kigeu geu. Mtu kama huyu kuwa Rais ni hatari sana. Kwa kauli yake mwenyewe alisema kamwe hataondoka CCM, tena akasisitiza kuwa mtu asiyemtaka ndio aondoke CCM. Lakini cha ajabu yeye ndio amekuwa wa kwanza kuondoka.
Leo hii anasema anataka kuwa rais ili awakomboe Watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini. Hivi kigeu geu kama huyu ambaye bado hajaupata huo urais ameshaonyesha kutoaminika na kauli zake mwenyewe, je, akiwa Rais tutaamini vipi kuwa hatageuka na kufanya mambo anayoyataka yeye kwa faida yake na marafiki zake ambao pasipo shaka wote tunajua kuwa ni wana shutuma za mafisadi kama yeye???? Hivi CHADEMA tutawaamini vipi tena kama wameshindwa kusimamia kauli zao sasa hivi, je itakuwa vipi hawa CHADEMA watakaposhika madaraka ya nchi na kuwa chama tawala??
Nimesikitika sana kuona chama nilichoamini kuwa ni chama bora cha upinzani sasa kimegeuka na kuwa pango la wanyang'anyi. Hivi inawezekana kweli mbwa mwitu akaingia kwenye kundi la kondoo na kuwa mchungaji wa kondoo na kondoo wakabaki salama??? Tuache ushabiki, tukubali ukweli, kwa hili CHADEMA wamechemka mbaya! CHADEMA wamewafanya Watanzania kama chapati.
Unaigeuza upande huu kisha unaigeuza upande wa pili au wamewafanya Watanzania kama samaki, unamla upande huu kisha unageuza upande wa pili pia unakula!
Ukweli ni kwamba kama itatokea Lowassa akashinda urais(ingawa naamini hawezi kushinda urais), ushindi utakuwa ni wa Lowassa na friends of Lowassa na hautakuwa ushindi wa CHADEMA.
Ushindi utakuwa ni wa Lowassa na familia yake na wale wote atakaotoka nao CCM. Lowassa atakuwa na kiburi mbaya sana sababu itajulikana wazi kabisa bila ya yeye CHADEMA si lolote, si chochote.
Ingekuwa bora mara elfu kama CHADEMA wangemsimamisha mtu mwingine mbali na Lowassa na kushinda uchaguzi hapa tungesema CHADEMA wameshinda urais.
Najua mpo humu ndani watu mtakao toa matusi na kashfa mbali mbali kuhusu mada hii. Lakini huo ndio ukweli, mpende, msipende CHADEMA sasa limekuwa pango la Mfisadi na wala rushwa, ambao wamekatwa na vyama vyao sasa wameamia CHADEMA ili wapate nafasi za kuendeleza matakwa yao binafsi.
Kwanini wasubiri kukatwa ndio wakimbilie CHADEMA??????
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments