[wanabidii] CHADEMA /UKAWA INAPASWA KUELEWA CCM BADO SIYO YA KUBEZA

Sunday, August 23, 2015

CHADEMA /UKAWA INAPASWA KUELEWA CCM BADO SIYO YA KUBEZA.

Kuna uwzekano CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani, chama ambacho kimeonyesha dalili kubwa ya kukamata dola kwa kuwahamasisha watanzania kuzijua haki zao, kikakwana kuyafikia malengo hayo. Katika siasa za Tanzania CHADEMA ndiyo chama cha upinzani ambacho kimeonyesha kukomaa kisiasa na hasa kuweka imani kubwa kwa wananchi weng.

Kwenye vita, huwa hairuhisiwi KUTOA MWANYA AU NAFASI YOYOTE KWA ADUI. Kuna wagombea ambao wameingia kwenye harakati kwa mikakati ya kujihakikishia AJIRA, wapo wagombea amabao wao kwao kuwa mbunge ni ili ajenge nyumba na kumiliki magari ya kifahari na kwao wao SIYO UTUMISHI wa umma, hawa wataigharimu CHADEMA. Sijui kama viongozi wa juu wanalijua hili? Kama wamelewa sifa za namna siasa zinavyoendelea na nguvu walizokwisha wekeza hasa za ushawishi kwa watanzania, nawakumbusha kwamba bado Chama cha mapinduzi siyo cha kubeza.

Siyo kazi rahisi kuiondoa CCM madarakani yenye mizizi tangu uhuru,yenye jeshi na usalama wa taifa, CCM ambayo haioni shida kumpa mgombea pesa ili ajitoe kama ilivyotokea huko Mtwara. CCM ni miongoni mwa vyama vikongwe katika siasa za Afrika na imekuwa ikishiriki kwa kiasi kikubwa kutoa ushauri juu ya namna gani vyama vingine vya nchi za nje vinaweza kuendelea kukaa madarakani. Kwa mfano CCM imekuwa ikishirikiana kwa karibu na chma tawala cha Zimbabwe katika kuhakikisha kinaendelea kukaa madarakani, hii inaonyesha ni namna gani kinajua mbinu za KUSHINDA UCHAGUZI MKUU.

Mpaka sasa kuna majimbo bado wagombea wa vyama vilivyokubaliana kuungana wanachukua fomu na kurudisha kinyume na makubaliano, hii inawachnganya sana wapiga kura wenu, mwisho wa siku watafikiri kumbe hata hawa ni kama walewale. Wapiga kura wanaandamana kupinga maamuzi ya vikao, ni vizuri kukaa nao na kuwaelewesha au kufanya maamuzi upya.

Hasa CHADEMA, imeonyesha ufa mkubwa ambao kwa haraka sana itatakiwa kuziba ili kubaki salama inapoanza kampeni za uchaguzi mkuu. Ufa huu ni namna ambavyo wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali wamepatikana, kuna MANUNG'UNIKO ambayo ni ya msingi kutoka kwa wanachama, mathalani, suala la kuwapitishwa wagombea ambao hawakupigiwa kura,masuala ya rushwa ndani ya uchaguzi pamoja na kulea makundi, tulishuhudia CHADEMA, ikishindwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la KALENGA, baada ya kumkata mgombea aliyepitishwa na kamati tendaji ya jimbo.

Pengine yaliyofanywa na CHADEMA kama chama kilichopewa ridhaa na wenzake wa UKAWA kwa nafasi kubwa ni sehemu ya kimkakati, katika kuyaokoa majimbo hayo ambayo kumetokea SINTOFAHAMU nyingi. Zipo taarifa za uhakika kwamba baadhi ya walioenguliwa ni mamluki ndani ya chama, lakini inahitaji dharula kuhakikisha ufa huu unazibwa katika kuhakikisha wanaingia kwenye mapambano bila mpasuko. INAWEZEKANA.

Baadhi ya wagombea ambao majina yao hayakurudi tena bila hata sababu za msingi kwa hao wagombea, ambao wengine wamekijenga chama kwa muda sasa, wameamua kujiunga na vyama vingine, ni haki yao kikatiba, lakini katika wakati kama huu ambao, kunahitajika umoja wenye nguvu zaidi haya hayakupaswa kutokea, pengine sasa CHADEMA inalewa sifa za umaarufu na nguvu waliyonayo.

Nafasi wanazozitoa zitawakatisha tamaa wanachama na wapiga kura, ama waipigie CCM au chama kingine au wasijitokeze kabisa kupiga kura.

Wanachama wapo katika sintofahamu, viongozi wapo kimya, huu ndiyo wakati ambao wapinzani wao wanautumia kuyanyakua majimbo yenye mpasuko na kata mbalimbali, na kupekea kutoa nafasi tena ya ushindi kwa CCM.

Binafsi Napata shida ninapoona yanayofanywa na CCM na pia CHADEMA yanafanyika, hii ni kukatisha tamaa wanachama na wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisubiri kuona CHADEMA, inawashughulikia wanaovuruga chama na kupenyeza mambo ambyo ni kinyume kabisa na utaratibu.
Ilitakiwa katika namna ile ile ambavyo CHADEMA imekuwa ikiwashughulikia wala rushwa na huko ndani mwao, ifanye hivyo, maamuzi ya ajabu yasiyo na maslahi ya wananchi hayakutakiwa kupewa nafasi kwenye chama hicho,kikongwe cha upinzani.

Ili UKAWA kupitia CHADEMA ishike nchi, inapaswa kuibomoa zaidi CCM, na kuhakikisha haitoi mwanya kwao, kujipenyeza katika namna yoyote ile, CCM, imekomaa sana haya yanayoendelea huko UKAWA yanaweza kutoa nafsi kwa CCM kwa kiasi kikubwa sana na kuua ndoto za MABADILIKO.

Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kuandika kitabu akiikosoa CCM, kile kitabu knaitwa TUJISAHIHISHE, huu ni muda wa kujisahihisha na kusonga mbele mkiwa wamoja zaidi ya sasa, ni muhimu kufahamu kwamba demokrasia na uelewa wa masuala ya kisiasa nchini mwetu inakuwa kwa kasi, wananchi hawa hawa mliozunguka nchi nzima kuwapa elimu ya uraia ndiyo watakao wapinga kwa nguvu pale mtakaposhindwa kujisahihisha. Imani iliyokwisha pandwa ndani ya mioyo ya wengi ikiondoka hakuna wa kuirudisha.
ZIBENI NYUFA ZILIZOONEKANA MAPEMA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments