[wanabidii] CHADEMA Tanga wamuunga mkono Slaa

Thursday, August 20, 2015
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoni Tanga kimesema kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu wanamuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu Dkt Wilbroad Slaa kwa kitendo chake cha kukaa pembeni kutokana na ujio wa Edward Lowassa na kupewa nafasi ya kuwania urais. 

Sisi wanachama na viongozi wa chama chetu mkoani Tanga tunaunga mkono kwa dhana kwamba kumsimamisha Lowassa kutaathiri mwenendo wa chama chetu kwa vile ndugu Lowassa haonekani vema na jamii kutokana na matendo yake Katika serikali ya CCM. 

Madai kwamba Lowassa amenunua nafasi ya Urais katika chama chetu kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 10 hayajakanushwa popote hivyo na sisi tunaona ni Madai ya kweli. 

Chama chetu kwa miaka kadhaa kimekuwa kikijenga kwa jamii kwa kueleza mabaya ya CCM ikiwemo suala la Katibu Mkuu kutamka majina ya watu 12 akiwemo Lowasa Kuwa siyo wasafi ni mafisadi katika list of Shame iweje leo awe mgombea wetu. 

Tusitishike na mikutano kujaa watu kwani wapo vijana ambao hawana shughuli za kufanya wanapenda mikusanyiko hivyo tusijifarague kuona tunaweza kushinda na mgombea huyu ambaye kule CCM katika vigezo 13 walivyoweka hakuwa anakidhi vipi sisi tumuone anafaa? 

Kwa kuwa michakato imeshafanyika kibabe na shinikizo la fedha sisi tutawapigia kura wagombea wetu wa udiwani na ubunge lakini Rais hatutampa mgombea wetu kwa kuwa hatoshi na hana sifa ya Kuwa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mwisho mwenyekiti kama una nia njema na chama kanusha suala la Lowassa kukupa fedha wewe binafsi vinginevyo huko twendako kwenye kampeni hoja hii itatumaliza na jamii iliyokuwa ikituamini kupoteza matumaini ya sisi kuwa Chama Tawala na hili tutawaumiza sana Watanzania ambao wamejenga matumaini kwa muda mrefu na sasa tumeharibu mwelekeo na matumaini yao. 

Jonathan Bahweje 
Afisa wa Chadema 
Kanda ya Kaskazini

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments