[wanabidii] CHADEMA MKOA WA MARA YATIMUA WAFUATAO

Friday, August 21, 2015
TANGAZO MUHIMU:

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO MKOA WA MARA KINAWAFAHAMISHA KUWA WAFUATAO WAMESIMAMISHWA NAFASI ZA UTENDAJI WA CHAMA NA KUWAVUA UWANACHAMA VIONGOZI WA WILAYA YA BUNDA KUANZIA TAREHE 15/08/2015

1. ALFRED SAMWEL IMANANI - MWENYEKITI WA JIMBO BUNDA 
2. RITHA SALVATORY IKANDILO - KATIBU WA WILAYA 
3. EMMANUEL MACHUMU MARIBWA - MWENEZI JIMBO
4. DAMAS KUNJU - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 
5. MWITA NG'WENA - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 
6. DICKSON KUJELWA - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 
7. DAVID ARBOGAST - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 
8. JUMANNE D. MOSSY - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 
9. NOAH LAWRENCE - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 
10. JACTON MUYENGI - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 
11. MATALA ATHUMANI - KATIBU BAVICHA KATA SAZIRA
SABABU ZA KUSIMAMISHWA KWAO NI:

1. Kumpiga na kumjeruhi sana aliyekuwa mtia nia wa jimbo la Bunda Mjini Ndugu Chacha Nyamhanga ambaye alilazwa kwa muda wa siku tisa katika Hospitali ya Wilaya ya Bunda. Sababu za kumpiga mtia nia huyo ni baada ya kukataa kutoa rushwa na kuhamasisha wenzake wasitoe rushwa kwa viongozi hao. 

2. Kuhujumu matokeo ya kura za maoni kwenye kata za Nyamuswa, Nyamakokoto, Nyasura, Manyamanyama na kufanya vikao vya uteuzi wa madiwani nje ya ofisi bila vikao vya kikatiba ili kuifanya CCM ishinde kata zote za Wilaya ya Bunda, mfano; kwenye kata Nyamakokoto walimteua ndugu EMMANUEL MALIBWA aliyepata kura 5 badala ya ndugu GEORGIES MIYAWA aliyeshinda kwa kura 37, Kata ya Nyasura aliteuliwa Jumanne Mosi aliyepata kura 17 na akaachwa Mwamba Wasira aliyepata kura 47. 

3. Kuiba mihuri ya Ofisi kwa lengo la kugushi nyaraka za chama. 

4. Kuwataka wagombea wa nafasi za udiwani kutoa rushwa ya kiasi cha shilingi laki tano ili waweze kuteuliwa na kamati tendaji kama wagombea wa nafasi hizo. 

5. Kuwasiliana na mgombea ubunge wa CCM Ndugu Steven Wasira kwa lengo la kuhujumu Chama ili mgombea huyo kutoka CCM apite bila kupingwa. 

6. Mwenyekiti wa Jimbo na aliyekuwa mtia nia wa ubunge Ndugu Ismail Pius Masululi amekuwa na mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ndugu Mirumbe kwa lengo la kuhujumu chama. 

7. Matumizi mabaya ya fedha za chama.

Ikumbukwe kuwa wakati wote wa uchaguzi majimbo yote ya Bunda huwa wanaikubali nguvu ya upinzani, na kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakikatishwa tamaa kwa vitendo vya viongozi wetu na wagombea kukiuza chama kwa Mhe Wasira, tumekuwa makini kuhakikisha hilo halitokei. Tunao ushahidi wa aliyekuwa Mgombea Ndugu Pius Masululi kununuliwa na Mhe Wasira kwa kiasi kikubwa cha pesa, baada ya kuona njama zake zimegundulika na jina lake kukatwa kaamua kuhamia CCM ambako ndiko alikuwa akitumika kwa muda mrefu. Tuna hakika ya kushinda majimbo yote Bunda baada ya waasi hawa kutolewa.

Tuma message hii kwa watu wengine pia kadili uwezavyo.
IMETOLEWA NA
KATIBU WA MKOA 
MARA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments