CCM TEMBEENI KIFUA MBELE, MALKIA WA MCHWA MLIEMCHIMBUA KAHAMIA UPANDE USIOWENU
Sote tunajua tabia ya mchwa na hasa wanapokuwa tayari wameshaweka ngome yao na KICHUGUU kuwa kikubwa. Ni kazi bure endapo utaanza kuhangaika na kuchimba CHUGUU zima ukifikiri unamaliza tatizo la Mchwa wanaokusumbua.
Dawa pekee ni kutafuta yule Mama kama siyo Bibi wa Mchwa wote walioko kwenye himaya hiyo, anaitwa MALKIA.
Hoyo ukishamuondoa , na tatizo limeisha, hutakaa uwaone Mchwa wala kile Kichuguu kikubwa hutokiona tena. Huyo ana tabia ya kufuata mwelekeo wa mwezi, mwezi ukiwa magharibi naye atakuwa upande huo, vivyo hivyo mwezi ukiwa Mashariki atakuwa mashariki, ni rahisi kutambua aliko.
Muhimu ni kwamba usipomuua yule Malkia ukamtupa tu , hafi na haumtupi peke yake, lazima atakwenda na Mchwa wengine wadogo wadogo na wakifika huko wataanzisha familia nyingine na muda si mrefu utashuhudia watu wa huko ulikomtupa wanaanza kulalamikia kusumbuliwa na MCHWA.
Hawa Mchwa wadogowadogo waliobaki CCM kama hawataamua kumfuata MALKIA, basi kazi ya kuwaua ni rahisi sana. Ni swala la subira tu, huko alikokwenda MALKIA, mapema tu tutasikia wanaanza kulia hasa ukizingatia kuwa MALKIA kabla ya kuondoka kwenda huko aliko sasa, alitengeneza Mchwa wadogo WATATU, ukijumlisha na aliotoka nao kwenu(CCM) hapana shaka majibu ya kuwepo kwa KICHUGUU tutayapata muda si mrefu.
0 Comments