KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WANAJESHI WASUMBUA TENA RAIA KIMBIJI-DAR
Wakazi wa kata ya Kimbiji wilayani Temeke nje kidogo ya jiji la Dar,
wamejikuta wapo katika mashaka ya maisha tena,baada ya baadhi ya
wanajeshi wanaodaiwa kuwa nania ya kuchukua maeneo wenyeji
kwa kutumia nembo ya kofia ya jeshi. wanajeshi hao walivamia maeneo
ya Kata ya Kimbiji/Ngobanya wakiwanyanyasa raia kwa kuwalazimisha
wahame katika maeneo yao.mkasa huo ulitokea siku ya jumapili ya 23 -09-2015,
Wakazi wa Kimbiji wamekuwa wakipata vitisho kutoka kwa baadhi ya
wanajeshi ambao wanataka kuchukua viwanja kutoka katika maeneo ya
raia bila ya ridhaa ya raia ambao ndio wenyeji wa eneo.
Wakazi wa kata ya Kambiji wanaiomba serikali kulinda masalahi na haki
za msingi za raia ambazo ni haki za binadamu kuliko kuwaacha baadhi
ya wanajeshi kusumbua raia.
Wakazi wakimbiji wanamiliki maeneo yao tangu enzi na enzi leo
wanajeshi wanapotaka kudhurumu ardhi raia wakaishi wapi?
wanajeshi wana eneo lao wamelipima kama shamba lipo Kimbiji/Kijaka sasa?
mbona wanasumbua raia !
VYOMBO VYA DOLA VINAOMBWA KULIINGILIA KATIKA SUHALA HILI.maelezo zaidi mwenyekiti 0713846688 au 0713768082
VYOMBO VYA DOLA VINAOMBWA KULIINGILIA KATIKA SUHALA HILI.maelezo zaidi mwenyekiti 0713846688 au 0713768082
0 Comments