[wanabidii] UKAWA SUMU HAIONJWI HATA SIKU, UKIONJA UTAKUFA TU

Sunday, July 26, 2015
Sasa ni karibia wiki ya tatu hivi tangu chama tawala kutangaza mgombea wake wa Urais, Mh. John Pombe Magufuli.

Hapo nyuma UKAWA walisikika wakitamba kuwa wanamsubiri kwa umakini mkubwa mgombea wa CCM, ili wajipange kumsambaratisha. Baada ya uteuzi wa mgombea wa CCM, UKAWA ni kama wameingia kizunguzungu na kigugumizi, maana mahesabu yao yamegota vibaya.

Kinachoonejana dhahiri ni kwamba uhai wa UKAWA unapewa uhalali tu na makosa ya chama tawala. Chama tawala kinapo weka mambo yao safi na kwa umakini, UKAWA wanaishiwa hoja na uhalali wa kisiasa, kwa vile wao wenyewe hawana unifying ideology, apart from being reactionary!

Tunachoshudia hivi sasa katika UKAWA, kushindwa vibaya kukubaliana juu ya mgombea wao urais ni kiekelezo tosha kuwa UKAWA ni utapeli wa kisiasa kati ya mambumbumbu wanao wania urais.

Hawajui nni awawakilishe na hawajui huko wanaenda kufanya nini.Hii ni hatari kubwa!

Watu wanaonadiwa na mamluki wa kibiashara inaelekea watainunua UKAWA wakati wowote ule na ni kwa nia moja tu, kukamata dili zote za dola ili wanufaike kiuchumi. Lakini wananchi makini wanaendekea kugutuka.

Tunajua kuwa hata wapinzani ni watanzania na huko kuna watu makini kitaifa.
Simpigii debe Dr Skaa lakini haingii akilini Dr Slaa kumtangaza Lowassa kuwa fisadi, halafu kula matapishi yake bila maelezo na kumkaribisha fisadi huyo huyo kukipigia debe chama chao.

Maendeleo ya Tanzania ni kuwa na upinzani makini utakao sahihisha kama sio kupiku chama tawala.Kwa ujinga huu wa kukumbatia ufisadi ulio temwa na chama tawala, UKAWA unawakaribisha kina Rosta na Karamaga and co. iliwagawane rasilmali za nchi hii.

Mungu bariki, mpaka hivi sasa ndani ya UKAWA ni mtafaruku wa kukaribia kusambaratika kwani hawajui wanaenda Ikulu kufanya nini na kwa madhumuni gani kwa mwananchi wa kawaida.

Sumu haionjwi

Share this :

Related Posts

0 Comments