Kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM kinakaa kuchuja kati ya majina yaliyofikishwa kwake na kamati kuu kuchagua 'tatu bora'. Wao wameletewa 'tano bora'.
Mtu ukiangalia nyuma na kuyaona matatizo yanayolikabiri taifa hili, hutakosa kuyaona. Kuna adui mkubwa aitwaye ufisadi. Huyu anajitokeza kwa sura nyingi. Kuna wanaoingiza taifa mikataba ya ajabu. Kuna watu wanawahujumu wengine ili mradi wanufaike wao, ndizo hizi capacity charges za ajabu. Kuna kupeana vyeo kwa maslahi binafsi. Kuna ukubwa wa serikali ambao ni mzigo kwa wananchi, Kuna marupurupu ya viongozi huku watendaji wakilipwa fedha isiyotosha hata kwa siku 15 kwa mwezi nakadhalika.
Kama mtu hujashawishika kwa namna yoyote na kambi yoyote katika uteuzi wa nani agombee au afikiriwe na chama kugombea unajua ni majina gani hayawezi kwa vyovyote vile kuwemo katika Tano Bora; naongelea uteuzi ndani ya CCM. Sasa kamati kuu (KK) imeleta majina matano kutoka katika orodha ya majina 38 ya wanaCCM waliorejesha form. Kama ilivyokuwa ikitarajiwa jina la Lowasa halimo katika tano bora. Tuliokuwa tunatetea maslahi ya taifa tumeona ahueni. Kama isivyotarajiwa jina la Membe limo katika tano bora. Kuna watakaoshangaa mimi kusema hivi maana huko nyuma nilimpigia debe membe. Lakini baada ya orodha ya 38 na hali iliyojitokeza tayari Membe alishakuwa kati ya shirini bora, wala si kumi. Ukiikumbuka orodha yote unasita na kujiuliza KK imetumia vigezo gani? Mizengwe? Kama ni mizengwe basin a Lowasa hakutendewa haki. Naogopa mizengwe hiyo inaweza ikaleta 'Bora tau' badala ya 'tatu bora'. Kama jina la Magufuli halitakuwemo basi tujue ni mizengwe. Na
hapo tujue hata CCM ina jina la Rais ajaye baada ya Membe. Itakuwaa sahihi kwa aliyesema jina la rais ajaye analijua Rais. Tulimbeza
Tuitembelee orodha ya watia nia? Hivi kabla KK ya kuwafikia Membe, Migiro, January iliwapitaje Mwandosya, Mwakyembe, Mwigulu, Pinda nk. Wajumbe wa Kamati kuu waliangalia nini na kuacha majina hayo mpaka wakaleta hayo? Kuna uwezekano mkubwa kuwa wameleta BORA TANO. 'Watanzania wanataka mabadiliko; wakiyakosa ndani ya CCM watayapata nje' alisema mwalimu Nyerere. Tutarajie mafuriko ambayo hakuna mwenye kiganja cha kuyazuia.
Elisa Muhingo
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments