[wanabidii] Nimesikitishwa na Freeman Mbowe kuuza CHADEMA kwa Edward Lowasa

Friday, July 24, 2015

Nimesikitishwa na uamuzi wa Freeman Mbowe kuuza CHADEMA kwa shilingi Bilioni 10 tu kwa Edward Lowasa

Nimepokea taarifa kwa masikitiko makubwa sana juu ya Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN AIKAEL MBOWE kuuza chama kwa shilingi bilioni 10 kwa fisadi Lowasa ambaye kwa mara kadhaa ametajwa kuhusika kwenye kashfa nyingi za ufisadi hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Edward Lowasa amempa Freeman Mbowe in personal shilingi Bilioni 10 kama hongo ili aweze kuteuliwa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA.

Hakika hizi ni taarifa mbaya sana kwa wapenda demokrasia nchini na kwamba vita dhidi ya ufisadi sasa inakuwa ngumu. Hii ni kwa sababu hawa wapinzani ambao ndio tuliwategemea kuiamsha serikali dhidi ya mapambano ya rushwa ndo wameingia kwenye mkumbo wa kutoa na kupokea rushwa. Hii ni fedheha kubwa sana kwao na ni aibu kwa siasa za Tanzania. Mbowe kanajisi upinzani na amedhalilisha sana siasa za nchi yetu.

Kwa Lowasa kuhamia upinzani si tatizo. Ila tatizo ninaloliona hapa ni hili la kutoa shilingi bilioni 10 ili tu ateuliwe kuwa mgombea urais. Kama kiongozi wa chama anaweza kununuliwa kwa shilingi bilioni 10, vipi kuhusu rasilimali za nchi yetu? Tutamtofautishaje na wale machifu ambao walikubali kuwekeana mikataba na wakoloni kwa kupewa tu bunduki, vioo na vipande vya nguo huku wao wakitoa vipande vya dhahabu? Hakika inaniuma sana na inasikitisha sana.

Ni dhahiri sasa hatuna upinzani wa kweli nchini bali tuna wachumia tumbo. Freeman Mbiwe pupa na tamaa ya fedha inamfanya asione azma aliyonayo juu ya maelfu ya wafuasi wake ambao walimuona kama ni kiongozi jasiri na mchukia rushwa. Sasa katumbukia kwenye shimo. Nani atamnasua? Tafakari na chukua hatua.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments