[wanabidii] kapumzike rais, Kikwete kiukweli umeyafanya yaliyowashinda wenzako,Magufuri ataendeleza ulipoachia

Sunday, July 19, 2015
Wakati muda wa kuelekea katika uchaguzi mkuu ukikaribia, watanzanzania tutamkumbuka sana rais Jakaya Kikwete kwa mambo mengi mazuri aliyotufanyia na uwazi wa serikali yake katika kushughulikia mambo mbali mbali ambayo viongozi wenzake waliotangulia hawakutubutu kuyashughuluika ikiwemo ufisadi serikalini.

Kwa wale watanzania waliokuwa hawana utamaduni wa kuweka kumbukumbu, wanaweza kukubaliana na dhana ya kuwa serikali ya Kikwete imekithiri kwa vitendo vya kifisadi ikilinganishwa na serikali zilizopita.

Binafsi napingana na dhana hiyo kwa kusema siyo kweli kwa kulinganisha baadhi ya mambo ya serikali hii inayomaliza muda wake mwezi October mwaka huu na serikali za marais wastaafu waliotangulia kwa wamu zote tatu.

Kwanza kabisa serikali ya kikwete imetujengea mfumo wa wazi wa uwajibikaji na ukweli usiofumbia macho jambo lolote wala kelele zozote zile zinazohusiana na ufisadi, pamoja na uwajibikaji wa viongozi wa umma na matumizi mabaya ya ofisi za umma.

Jambao la pili serikali ya rais Kikwete, kwa kipindi cha chote cha miaka 10, imeyakataa kupuuza kila aina yeyote ya tuhuma zinazoibuliwa na vyombo vya habari au wanasiasa kutoka kambi ya upinzania au hapa ndani ya ccm yenyewe tofauti na awamu zilizotangulia.

Rais kiwete kwa utashi wake amekataa kabisa kujiingiza katika mtego wa kuwalinda watendaji wa chini dhidi ya tuhuma na kelele zinazopigwa juu yao na amekuwa akichukua hatua stahiki pale wanapokutwa na hatia.

Wakati wa utawala wa awamu ya pili, kuna mabilioni ya fedha yalitolewa na wafadhili kwa serikali kwa ajili ya kuwakopesha mitaji wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, maarufu kwa jina la OGL. Mzee Mrema anaujua vizuri mfuko huo wa OGL na malengo yake.

Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara wanaojinasibu na uzawa, kwa kushirikiana na wafanyabiashara kutoka nje wakiwamo kina Chadva, walijichotea mabilioni ya shilingi kwa kisingizio cha kufufua zao la mkonge. Lakini hakuna mkonge uliofufuliwa.

Baadhi ya magazeti na wanasaiasa tena wengine wakiwa serikali akiwemo mzee Mrema walipiga kelele sana kuhusiana na kasha hiyo lakini, lakini hakuna mtendaji wala waziri aliyechukuliwa hatua au kuwajibika kutoka na kulindwa kwa mfumo wa serikali iliyokuwepo.

Chini ya utawala wa Benjamini Mkapa kuna kashfa kubwa mbili ununuzi wa rada na ndege ya rais. Rada hiyo hiyo inayoendelea kufanya kazi kwa kusuasua hadi sasa pale uwanja wa ndenge wa kimataifa wa Mwl. Nyerere .

Vyombo vya habari licha ya kupiga kelele pamoja na wanasiasa wa vyama vya upinzani kuhusu kashfa zote mbili lakini wahusika waliendelea kulindwa na mfumo ulikokuwepo, madarakani hakuna hata mmoja aliyewajibika.

Pamoja na waziri mambo ya nje wa Uingereza, Clara Short kujiuzulu kutokana na kitendo cha serikali yake kuiuzia nchi masikini ya Tanzania rada kwa bei ghali mara mbili ya bei yake halisi lakini hakuna waziri wala mtendaji aliyewajibishwa na mamlaka ya uteuzi kama anavyofanya leo Rais Kikwete.

Hata kashfa ya EPA imekuja kushughulikiwa na rais Kikwete, haliyakuwa ilitendeka wakati wa rais Mkapa na kutokana na mfumo wa usiri uliokuwemo serikali kashfa hiyo haikuweza kugundulika hadi alipoondoka madarakani na kuingia serikali ya Kikwete iliyozingatia mfumo wa uwazi na uwajibikaji.
Jambo la tatu kabla ya rais Kikwete, ripoti zote za CAG, ziliishia kwenye makabati ya ikulu. Lakini baada ya Kikwete kuingia madarani, aliagiza ripoti zote za CAG,zijadiliwe bungeni kwa uwazi ili wananchi wafahamu uozo uliopo ndani ya serikali yao, na zaidi ya hapo bunge likapewa uhuru wa kupendekeza hatua za kuchukua dhidi ya watendaji wa serikali ambao ripoti ya CAG, zimetaja kukithiri kwa uozo katika maeneo yao.

Jambo la nne kabla ya rais Kikwete, Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (Takukuru) ilikuwa haina uwezo wa wala mamlaka ya ya kuchunguza na kumfikisha mahakamani mtuhumiwa.
Kabla ya rais Kikwete taasisi hiyo iliishia kuchunguza tu na kupeleka taarifa ofisi ya rais kwisha hab ari yake na muamuzi wa nini kifanyike alijua rais tu.

Jambo la tano kabla ya rais Kikwete, taasisi za serikali na mashirika ya umma pamoja na halmashauri zilikuwa zina uwezo wa kupeana kazi na kulipana na wazabuni kiholela kwa njia ya kifisadi, Leo hii hakuna fedha ya yeyote ya serikali , taasisi, mashirika ya umma pamoja na halmashauri yeyote nchini inayoweza kulmlipa mzabuni zaidi ya shilling milioni 10 bila kupitia benki kuu (BOT) kwa lengo la kuhakikiwa uhalali wake.

Jambo la tano Serikali ya rais Kikwete imetoa uhuru mkubwa kwa vyombo vya habari na mitandao ya jamii, katika kuibua kashfa na ufisadi mbalimbali na hakuna kashfa wa ufisadi wowote ulioibuliwa vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ambayo haikufanyiwa kazi wala kufuatiliwa na serikali yake.

Jambo la sita ukiziacha tawala zote tatu zilizopita kabla ya rais Kikwete hakuna utawala ambao ulioagiza wizara zote pamoja na taasisi za umma kuwa na kitengo cha mawasiliano ya umma kinachoongozwa na maafisa wa habari wenye taaluma ya uandishi wa habari, ambao moja ya wajibu wao mkubwa ni kuwa na mawasiliano na vyombo vyote vya habari hapa nchini pamoja na mitandao ya kijamii kuelezea kinachoetendeka ndani wizara au taasisi zao.

Kwa hiyo kelele zote za zinazopigwa dhidi ya serikali yake na vyombo vya habari, wanaharakati na wanasiasa kuhusu vitendo vya ufisadi katika serikali yake yakuwa inaongoza kwa kuwawajibisha watendaji wake wakiwamo mawaziri hiyo inatokana na mfumo mzuri wa uwazi na uwajibikaji aliouwasisi rais Kikwete mwenyewe.

Mwisho ni kumpongeza rais Kikwete na tunamatumaini na John Magufuli kuwa atakayeendeleza dhana ya uwajibikaji katika kukabiliana na aina yeyote ya ufisadi nchini, na kuondoa dhana kuwa wakubwa huwakingia kifua watendaji wa chini yao wanapotuhumiwa kwa jambo lolote lile.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments