[wanabidii] hongera Muhimbili mmethiubutu na mmeweza

Tuesday, July 21, 2015
mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za afya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwamba sasa, wagonjwa wenye matatizo ya moyo wataweza kufanyiwa uchunguzi na kuweza kuhudumiwa kwa kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo kwa mfumo wa kisasa zaidi.

Kwamba wagonjwa wenye matatizo hayo ya moyo, wataweza sasa kuzibuliwa matundu hayo kwenye moyo bila kufanyiwa upasuaji kifuani. Hii, kwa hakika ni habari njema, tena yenye kustahili kupongezwa.
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mafanikio haya, ni kwamba kufungwa kwa mtambo maalumu Hospitali ya Taifa Muhimbili, "Cath Lab" ndiko kutafanikisha huduma hizo muhimu katika maisha ya binadamu.

Kwa ufafanuzi tu ni kwamba, Cath Lab ni mtambo maalumu unaotumika kufanya uchunguzi, kuzibua mishipa inayopeleka damu kwenye moyo na kuziba matundu ya moyo bila kufanya upasuaji.

Kwa kuzingatia ukubwa wa magonjwa ya moyo nchini na gharama ambayo serikali na hata watu au taasisi binafsi zimekuwa zikiingia kusafirisha wagonjwa wa moyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao kwa tiba za aina hii nje ya nchi, hakika, kwa kiasi kikubwa hatua hii itasaidia kuipa sura mpya sekta ya afya hapa nchini.

Tunajivunia wataalamu wetu nchini ambao tayari wameutumia mtambo huu kwa ufanisi mkubwa, kupitia Kitengo cha Tiba ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakifanikiwa kufanya tiba ya moyo kwa kuziba matundu ya kwenye moyo bila kufanya upasuaji wa kifua.

Lakini si tu wataalamu wetu hapa nchini bali hata wenzao kutoka nje ya nchi ambao, kwa pamoja, wamefanikisha tiba hiyo, hao ni pamoja na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre ya Riyadh Saudi Arabia.

Tunaungana na Watanzania wengi katika kuamini kwamba hi ni hatua nyingine kubwa katika nyanja ya tiba na afya nchini baada ya kushuhudia ushirikiano wa aina hii na hospitali nyingine kadhaa za kimataifa kwa kutumia mifumo ya habari kama Video Conference ambayo huwawezesha madaktari kufanya upasuaji nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa wenzao walioko nje ya nchi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments