[wanabidii] ESCROW ILIIUMIZA CCM: KUWAFUKUZA WABUNGE KUTAIUMIZA ZAIDI

Wednesday, July 08, 2015
Wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakajana kulikuwa na hasira za wananchi juu ya sakata la ESCROW na ufisadi wake wote. Watanzania walikasirika na kukiumiza Chama Tawala katika uchaguzi huo. Licha ya mbinu za kihuni kama kutangaza walioshindwa kushinda, lakini bado CCM iliumia na kila mtu anajua. Nakumbuka mtu mmoja kuniuliza kwa nini CCM kushindwa hivyo? nikamwambia ESCROW. Akabisha. baadaye alikubali. Yeye hakuamini kuwa vijijini watu wanao uelewa wa kutafsiri jambo hilo. Kituko cha Speaker kuwafukuza wabunge wa Upinzani katika bunge linaoishia, na kupitishwa kwa miswada ya sheria yenye utata kimewakasirisha watanzania na zaidi vijijini kuliko inavyoweza kuaminika. Tayari watu wameanza kuonyesha hasira zao juu ya jambo hili. Wameapa kutokosea kupitia uchaguzi. kuna wagombea watarajiwa wa CCM wameaza kusutwa. Wanasema wana uhakika CCM iliwafukuza wabunge hao ili kupitisha madudu. Wanasema kuwaachia uongozi ni hatari. Kuna wanaodhani Makinda
(Speaker Anna) kakusudia kukisaliti chama chake kupitia njia isiyoweza kudhaniwa. Ni matumaini yangu kuwa Chama kupitia kwa wasemaji wake Nape na katibu mkuu watalisawazisha. Wakilidharau wasilaumu na wajue litatumiwa. Miswada imeanza kujadiliwa. Nimesoma mahala kipengele kinachosema mikataba ya zamani haitarekebishwa. hayo yakitumiwa na upinzani CCM iwe tayari kwa lolote.
 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments