[wanabidii] Edward Ngoyai Lowassa Kuitosa CCM ?

Monday, July 13, 2015
Mwanasiasa Edward Ngoyai Lowassa ambaye yupo katika sintofamamu na chama chake CCM atazungumza na waandishi wa habari leo au kesho nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam iwapo atawahi kumaliza kikao na familia yake.

Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa mtoto wa Lowassa Fredy Lowassa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zake za kuelekea Urais kwa tiketi ya CCM zinaarifu kuwa Lowassa alianza kwa kufanya mazungumzo ya kina na familia yake huku katika kikao hicho Watoto wake wote wakihudhuria lakini pia wakwe zake akiwemo Sioi Sumari na kukubaliana baadhi ya mambo.

Mambo yanayodaiwa kukubaliwa na wanafamilia hao ni kwamba wawe tayari kumfuata katika chama chochote atakachoamua kuelekea, huku akishindwa kubainisha ni wapi atakapoelekea kwani alisisitiza kuwa hawezi kuhama au kutangaza uamuzi wowote pasipo kushauriana na marafiki zake wa karibu.

Hivi sasa waandishi wa habari wamefika nyumbani kwake Masaki hata hivyo wameombwa kuondoka na kuwa na subira kwani Lowassa bado anafanya mazungumzo na marafiki zake muhimu. mashuhuda kutoka eneo la tukio wanadai moja kati ya magari ya watu waliopo Nyumbani kwa Lowassa yameonekana kuwa ni yavmwenyekiti wa ccm wanawake taifa Sophia Simba, Lawrance Kago Masha, Adam Kimbisa, Emmqnuel Nchimbi, Mwenyekiti wa vijana taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge zanzibar Sadifa Khamis, Hussein Bashe, Absolomon Kibanda, Khamis Mgeja(mwenyekiti ccm Shinyanga) Msukuma(mwenyekiti ccm Geita), Na Mgana Msindai(mwenyekiti CCM Singida).

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments