[wanabidii] CHADEMA: 'Lowassa siyo fisadi', CCM: 'Lowassa ni fisadi'

Monday, July 27, 2015

CHADEMA: 'Lowassa siyo fisadi', CCM: 'Lowassa ni fisadi'

Waziri Mkuu wa Uingereza aitwaye Harold Wilson aliwahi kusema, A week is a long time in politics.

Watanzania tumejaliwa kila kitu cha kidunia mpaka unafiki na usahaulifu!

Septemba 15, mwaka 2007, Dk. Slaa alisimama jukwaani na kutangaza orodha ya mafisadi 11 katika mkutano ulioitishwa na vyama vya upinzani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. Mojawapo katika majina hayo lilikuwepo jina la Edward Lowassa.

Baada ya kutangaza, WanaCCM wengi walipinga kwa nguvu zote wakidai huo ulikuwa ni udaku huku wakitaka vielelezo vya ufisadi kuonyesha ukweli wa kile CHADEMA walikuwa wanakisema.

Miaka minane baadaye, wale wale waliosimama kwenye majukwaa na kudai Lowassa ni fisadi, kwa sasa wameanza tena kupiga kelele kuaminisha Watanzania wakidai Lowassa siyo fisadi, wakati huo huo, CCM nao wamebadilika na kuanza kupiga kelele wakidai Lowassa ni fisadi. CHADEMA nao kwa sasa wanaomba vielelezo vya ufisadi wa Lowassa.

Watanzania wengine wanajiuliza, what's going on?

Wanaopiganiwa kwa sasa wako kimya huku nyasi zikiumia!

This is more than political flip-flop!

Waingereza wanasema, money talks and money alone sets the entire world in motion!

Ama kweli, a flag follows the direction of the wind!

Siasa za aina hii zitaendelea kulitafuna taifa wakati wachache wakifaidika kwa unafiki na ufisadi.

Share this :

Related Posts

0 Comments