Sitta alisema hayo jana wakati akizungumza na makada wa chama hicho waliojitokeza kumdhamini katika wilaya ya Geita mkoani Geita na kusema kuna baadhi ya watia nia wanaopita wakisema kuwa wakiwa marais watapambana na rushwa wakati ukiwatazama macho yao yanaonyesha ni wala rushwa. Viwango vya kubadili fedha za kigeni, kwa sasa Dola moja ya Marekani sawa na Sh2,000.
"Nilitumwa Canada kutafuta ndege tatu, jioni moja tukiwa Canada tunajiandaa kuondoka, akaja mkurugenzi wa masoko wa kampuni tuliyonunua ndege, akaniambia waziri tuna kautaratibu hapa ukifanikisha ndege zetu zikanunuliwa tunatoa bakshishi ya Dola 70,000 utataka hizi hela tuzipeleke benki gani," alisema Sitta akimnukuu ofisa huyo wa masoko.
"Watazameni hawa watu... mtu kawa waziri mwaka mmoja leo anataka urais, halafu anasema atapambana na rushwa...utapambana na rushwa wapi wakati hata hujapita kwenye mitego ya rushwa. Watazameni kwa makini, mtawajua tu kwa macho, kwani macho yao yamekaa kijanjajanja kweli," alisema. Aliendelea, "Kwa kuwa mimi nililelewa vizuri nilijua tu huo ni mtego wa shetani, nikamwambia mkurugenzi nitampa jibu kesho, nikawasiliana na wakubwa zangu kwanza wakakubali ni chukue hiyo pesa ikasomeshe marubani wa ndege."
Sitta aliwataka wananchi hao kuwatazama kwa makini watangaza nia hao, na kuwauliza iwapo tayari walishawahi kupambanishwa na rushwa.
Chanzo Mwananchi
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments