Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Rais Kikwete alisema kikao cha Halmashauri Kuu kina umuhimu wake kwa sababu kitaamua ushiriki wa CCM katika Uchaguzi Mkuu na kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea wa chama hicho.
Rais Kikwete alisema watu wote wanachama na wasio wanacham wanasubiri kwa hamu uamuzi wa vikao vya juu vya CCM.
"Watanzania wote bila kujali itikadi zao wanaitazamia na kuitumainia CCM kutoa uongozi ulio bora kwa nchi yetu. Hali hii inathibitisha uleusemi wa Baba wa Taifa kwamba Rais anaweza kutoka chama chochotelakini rais bora atatoka CCM," alisema.
Alisema CCM inatakiwa kutambua na kuzingatia uzito wa wosia huo wBaba wa Taifa na kuhakikisha kuwa unatekelezwa kwa ukamilifu wake.
"Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Vikao vya Kamati Kuu, HalmashauriKuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa, vina jukumu maalumu la kuongozna kusimamia mchakato wa uteuzi ndani ya chama, utakaotuwezeshkupata wagombea wanaofaa,"alisema.
"Wenye kukidhi kiu na matarajio ya wanachama wa CCM na wananchi waJamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni sisi. Lazima tupate wagombewanaochagulika, tunapowapeleka kwa wananchi ambao wengi wao siywanaCCM."
Alisema CCM wako milioni sita lakini wapigakura ni milioni 23, kwa hiyo lazima wapate mtu ambaye wananchi watamkubali.
Rais Kikwete alisema wakimpata mtu ambaye wao CCM inampenda, lakinwananchi hawatampenda, chama hicho kitaumia."Lazima tupate wagombea ambao wananchi watasema 'naam', tusipatwagombea ambao watu wataguna. Watasema 'eeh yaani CCM wamemleta huyu? Tutauweka ushindi kwa CCM rehani. Ndugu zangu lazima tutambue kuwa wakati umebadilika,"alisema.
"Ni ngumu sana kwenye chama chetu ukiwaambia kuwa wakati umebadilika na tunaweza kushindwa, wanakuwa wagumu sana, lakini mnajidanganya tu,
lazima tujue kwamba wakati umebadilika… ile dhana kuwa yeyotatakayeteuliwa na CCM atashinda imeshapitwa na wakati."
Rais Kikwete alisema dhana ya kuwa wakichagua mtu yoyete mradi katokCCM, watakuja kukiona cha mtema kuni.
"Hivyo ni lazima tupate wagombea wanaochagulika na wananchi ambao niwengi kuliko wanaCCM. Hatuwezi kupeleka kwa wananchi watu wasiokubalika, watu waliopungukiwa sifa, tukadhani Watanzania watamchagua tu kwa sababu ni mgombea wa CCM,"alisema.
"Lazima tuwe na wagombea watakaopendeza kwetu na watakaopendeza kwa Watanzania. Wagombea ambao watu wataamini kuwa wako salama, nchi,jimbo, kata zipo katika mikono isiyokuwa na shaka."
Alisema wakipeleka wagombea wanaowapendeza wao bila kuwapendeza wananchi, watakula hasara.
"Tutajipa kazi kubwa ya kufanya na kuna hatari ya kushindwa. Lazima tusome alama za nyakati. Tutambue zaidi watu wanachukizwa na watu wa namna gani? Tusipeleke mtu anayeakisi mambo yanayochukiza watu na kujiaminisha kwa historia na nguvu ya Chama cha Mapinduzi atashinda hampiti nimesema wakati ule ndugu zangu umekwisha,"alisema.
"Tusidanganyane kwamba sisi tunapendana au tunaogopana, wananchi hawatatuogopa. Wananchi hawatakuogopa wala hawatasita kuonyesha kwamba hawapendezwi naye. Tukifanya uteuzi mbaya wa wabeba bendera kwa urais, wabunge wawakishi madiwani hasira za wananchi zinaweza kuwa kwa chama kizima na kuadhibu wagombea wetu ngazi nyingine."
Alisema wakipata mgombea ambaye wananchi wataguna, wananchi wanaweza wakapata hasira na wakawakataa wagombea wote.
Rais Kikwete alitoa mfano wa chama cha nchini Canada ambacho kilikuw kikiongoza tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia, lakini kilipoenda katika uchaguzi kikashindwa hata kuwa chama kinachoongoza katika upinzani ndani ya Bunge.
"Ndiyo maana nasema sisi tusilewe historia kwamba chama kikubwa.
Tukifanya makosa hatutafika. Tusikubali kukifikisha chama chetu hapo kwa sababu ya urafiki. Chama kwanza, mtu baadaye," alisema.
Alisema bahati nzuri CCM ina misingi mizuri ya kupata wagombea wake,labda waamue wenyewe kutoiheshimu misingi hiyo ambayo imejengwa katikkanuni na taratibu za kuwapata wagombea.
Rais Kikwete alisema CCM ina maadili na miiko yake ya kuzingatia taratibu na kwamba miiko hiyo imejaribiwa na kutumika na kuwapata wagombea wazuri waliokiletea chama ushindi na heshima katika chaguzi zilizopita.
"Nawaahidi hatutayumba wala hatutaogopa katika kusimamia misingi hii mizuri ya chama chetu, kwa nia ya kukumbushana dhima na wajibu wwanachama na viongozi tulio nao katika kulitekeleza hili," alisema.
Aliwataka kuongozwa na kuweka masilahi mapana ya chama chao, kulikmasilahi ya mtu mmoja mmoja.
"Nayasema haya kwa sababu naona kumekuwepo kujisahau au kujifanya kuwa umesahau miongoni mwa wagombea wa uteuzi na hata miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu na viongozi wengine wa chama na hatwanachama kwa kufanya mambo mengine yaliyo kinyume na misingi ychama," alisema.
"Tusitoe nafasi ya kukimong'onyoa chama, haiwezekani yanaposema aminaposikika minong'ono baina ya wagombea, washabiki na baadhi yettukiwemo humu (Nec), hayanifurahishi hata kidogo."
Alisema watu kufanya mambo yaliyo kinyume na uteuzi ndani ya chama mambo yasiyokubalika, hayataachwa yapite.
"Naomba myazingatie ili mrahisishe kazi ya uteuzi, tujadili tu historia ya mtu na uwezo wake kwa nafasi anayoiomba. Isiwe tunapoteza muda mwingi kujadili makando kando, mambo yanayofanyika kinyume cha utaratibu. Utafanyaje mambo kinyume cha utaratibu unataka kukipeleka wapi chama chetu?
"Mnataka iweje, tuseme hakuna kilichofanyika? Haiwezekani hatuwezi
kunyamaza tutakuwa tumepoteza dhamana yetu. Tunao wajibu wa kusimamia misingi tuliojiwekea na kikao hiki ndicho chenye dhamana hiyo,alisema.
Alisema wamedhamiria kusimamia bila ajizi, bila kupendelea na kwamba wana wajibu wa kutenda haki na watafanya hivyo na bila shinikizkutoka kwa mtu yoyote.
"Bila shaka viongozi wenzangu tumeelewana, tusaidiane ili tuvuke vyema," alisema.
Alisema Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 bado inaandaliwa na imefikia
mahali pazuri na kwamba kikao kijacho itapelekwa.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments