[wanabidii] Namna ya kuongeza ufanisi katika biashara na maisha yako kwa asilimia 100%

Tuesday, June 23, 2015


Watu wengi ninaokutana nao katika ushauri wamekuwa wakiniuliza kwamba, Jee wafanye nini ili kufanikiwa katika shughuli zao hasa za biashara? Napenda kuwapatia jibu lifuatalo, ili ufanikiwe unapaswa kufanya mambo yafuatayo;
KUWA NA MALENGO
Ili ufanikiwe maishani unapaswa kujiuliza jee unataka nini maishani? Unapaswa kuwa na malengo hasa ya kiuchumi. Jiulize sasa hivi una kipato gani kwa mwezi na kwa mwaka? Jee miaka 3 hadi 5 ijayo unataka uwe na kipato gani kwa mwezi na kwa mwaka? Ili uongeze kipato kwa sasa ni kitu gani (kimoja) unapaswa kukifanya ambacho kinaweza kubadilisha maisha yako. Orodhesha mambo 10 ambayo unalenga kuyafanya halafu uchague jambo moja tu ambalo ukilifanya linaweza kubadilisha maisha yako. Mbinu hii imebadilisha maisha ya watu wengi kwa haraka sana.

MAMBO MENGINE UNAYOPASWA KUYAFANYA ILI UPATE MAFANIKIO YA HARAKA

-Unatakiwa kuwa na mwalimu Business Coach/ Mentor. Kama ilivyo katika maisha na hata kwenye michezo wanamichezo waliofanikiwa hasa kwenye michezo kama soka, wanasoka wengi waliofanikiwa wamepitia kwenye shule bora za soka na wamefundishwa soka na makocha wazuri. Vivyo hivyo hata katika biashara hasa katika nchi zilizoendelea wajasiriamali wengi waliofanikiwa wamepitia chini ya makocha wa biashara. Mfano Anthony Robins alifundishwa ujasiriamali na Jim Rohn. Maendeleo ya taifa la Marekani katika ujasiriamali yanatokana na kuwa na walimu wengi wa ujasiriamali ambao wao pia ni mamilionea na wanafundisha kitu wanachokijua na wanachokitenda. Kuwa na kocha kunakusaidia kujifunza haraka na kuepuka makosa ambayo ungeyafanya kwa kutokuwa na kocha. Kwa hapa Tanzania Kampuni ya CPM Business Consultant imeamua kuanzisha utaratibu huu bure bila malipo yoyote kwa kushirikiana na Mentor wetu ambaye ni mfanya biashara maarufu anayemiliki kampuni kubwa ya clearing and forwarding. Tunaendesha mafunzo ya Mentorship kwa email au na kwa kuendesha semina kila siku ya jumapili saa 10.00 jioni, Kimara Baruti kwenye ukumbi wa Bahama mama. Kujiunga na mpango huu au kupata maelezo zaidi unaweza kunipigia simu namba 0784394701 Au tembelea tovuti hii kujiunga na mafunzo haya;http://tinyurl.com/freementorshiptz


- Unatakiwa kupata mafunzo ya ujasiriamali kwa njia ya kuhudhuria semina, kuangalia Video au kusikiliza Audio books.Kuzipata semina za ujasiriamali unaweza kutembelea mitandao ya kijamii kama vile facebook,Jamii Forums na Wanabidii forums utaona matangazo ya semina za ujasiriamali. Mahali ambapo unaweza kupata video au Audio books wasiliana na mimi nikuonyeshe mahali pa kuzipata kwa bei nafuu ya sh. 20,000 tu. Video/Audio books hizo unaweza kuziweka kwenye flash,Laptop au kwenye simu yako. Unaweza kuwa unazisikiliza ukiwa kwenye gari lako ukienda kazini ukiwa kwenye mazoezi au unasubiri kwenye foleni mahali ukisubiri huduma. Utajifunza mambo mengi sana kwa muda mfupi kutoka kwa magwiji wa maswala ya ujasiriamali ulimwenguni. Hii ni sawa na kupata semina kutoka kwa makocha wa ujasiriamali/mentors kutoka Marekani ukiwa hapa hapa Tanzania au sehemu yoyote ulimwenguni. Ili kupata Audio books wasiliana na mimi kwa simu namba 0784394701.


- Ili kufanikiwa katika biashara zako unapaswa kuwa na vyanzo vingi vya mapato mfano; Unaweza kuanzisha biashara yako,kuwekeza kwenye majengo (real estate) unaweza kufanya biashara ya mtandao(Network marketing) unaweza kuwekeza kwenye akaunti maalum au kwenye hisa. CPM Business Consultants inafundisha jinsi ya kufanya mambo hayo yote.
-Unapaswa kujifunza namna ya kutumia muda wako vizuri(Proper Time Management).
- Mwisho kabisa kama wewe ni mwajiriwa tutakufundisha namna ya kuongeza ufanisi sehemu yako ya kazi.

Mwandishi wa makala hii ni Mshauri wa biashara na Mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara. Jee unapenda kujiunga na Mafunzo ya namna ya kuongeza ufanisi katika biashara na maisha yako kwa asilimia 100% Piga simu namba 0784394701.Au tembelea tovuti hii kujiunga na mafunzo haya; http://tinyurl.com/freementorshiptz
CHARLES NAZI
MKURUGENZI MTENDAJI
CPM BUSINESS CONSULTANTS


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments