Akitangaza nia yake katika eneo la Mwitongo kijijini Butiama jana, Makongoro aliwashambulia makada wenzake ndani ya CCM ambao wanaongoza makundi ya kuwania urais kwa kuwaita ni 'vibaka' wanaokivuruga chama hicho kwa maslahi yao binafsi.
Akitoa mfano kwa baadhi ya makada wanaoongoza makundi ndani ya chama hicho, Makongoro aliwataja kwa majina kuwa ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira.
Alisema makada hao kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kuendesha makundi ya urais na akahoji sababu za kutafuta cheo hicho cha juu kwa fedha.
CCM irudishwe kwa wazalendo kwa sababu vibaka wamekuwa na mlengo mbaya wa kukiendeleza chama hicho, alisema.
Alisema ndani ya chama hicho kumekuwa maradhi ya rushwa ambayo yameiambukiza nchi nzima.
Alisema ndani ya chama hicho kumekuwa maradhi ya rushwa ambayo yameiambukiza nchi nzima.
Makongoro alisema yeye ni mzalendo wa kweli na anataka kuirudisha nchi katika misingi ya uadilifu endapo CCM itampa ridhaa ya kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Alisema ndani ya chama hicho kumekuibuka genge la watu wachache ambao utajiri wao ni wa shaka na umejijenga kwa fedha chafu.
"Ndani ya chama tawala wamekuwapo 'vibaka' wachache… unajua kibaka ni kibaka tu hata kama kapewa gari la Serikali lina bendera ya taifa mbele atabaki kuwa kibaka tu.
"Wananijua vizuri huwa siwaonei haya kuwaambia ukweli, hawa ndiyo wanaotuvurugia chama na hawamheshimu Mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete," Makongoro.
Katika hotuba yake ambayo alitumia saa mbili, Makongoro alijikita kuzungumzia madhara yanayotokana na rushwa ndani ya CCM na alisema baadhi ya makada wanaotumia rushwa wamezalisha makundi na mipasuko isiyo ya lazima huku akisisitiza kuwa anachukia kuwapo makundi ndani ya chama hicho.
Kwa mujibu wa Makongoro, hali hiyo imechochea badhi ya viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali wakiwamo wenyeviti wa mikoa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kuishi kama mifugo.
Alisema hali hiyo imesababisha baadhi ya viongozi hao kuishi maisha ya kusukumwa kwa upepo wa makundi yanayomilikiwa na watoa fedha.
Aliwaasa Watanzania wawaogope watu wanaoonekana kuwa na haraka ya kukimbilia kutawala nchi.
"Ukiona watu kazi inatangazwa ifanywe kwa utaratibu wake na mtu aliyeiomba kazi hiyo anakiuka taratibu, muogopeni sana huyo hafai kukukuongoza maana hata akikuongoza ataendelea kukiuka taratibu ili ajinufaishe," Makongoro
0 Comments