(Dr.Muhammed Seif Khatib)
Utamaduni kwa mawazo ya Mswahili ni ngoma.Wapo wanaoihusisha ngoma hiyo na mzunguko wa kiuno na kibwebwe.Bila kukatw viuno ngoma hainogi.Wapo wanayohusisha
tafsiri ya Utamaduni na ngoma ya kutikisa na kuzungusha mabega.Wengine ngoma kwao ni
kupiga makofi na kusakata miguu.Ngoma kwa Wengine ni kushika silaha na kuruka hewani.
Utamaduni kwa wengine wanahusisha mitindo ya mavazi ya asili, vyakula na matambiko.Taratibu za harusi, posa,tanaka na Mahari uhusishwa na tamaduni.Vyakula navyo
uhusishwa na Utamaduni wa watu na jamii yenyewe.Yawezekana mambo hote hayo yakahusishwa na maana pana ya utamaduni. Utamaduni unaweza kutafsiriwa kuwa ni mila,
desturi na silka za watu wa jamii fulani.Ni utaratibu uliojijenga kwa jamii ya watu ya kufanya
mambo kwa vigezo maalumu.Vigezo vinavyomwongoza mwanajamii kuishi kwa kufata taratibu
zinazokubalika na jamii hiyo.Taratibu hizo hukomaza tabia za watu wa jamii husika na baadaye
kuonekana katika kufanana na wanajamii hiyo.Hukusikia watu wengine endapo mtu akifanya
Jambi ovu katika jamii huambiwa ' huu siyo Utamaduni wetu'. Hata katika maisha ya makabila
huonekana utamaduni maalum kwa watu wa kabila inayohusika.Lakini mataifa ya dunia yapo
mambo yanayofanana ya watu wa taifa Hilo ambao ndiyo utamaduni wao. Kwa muktadha huu
twaweza kusema upo Utamaduni wa jamii, kabila au taifa.Ni utamaduni uliojengwa kwa muda
mrefu na hatimaye sehemu ya maisha na tabia ya watu wa taifa linalohusika.Jee, Watanzania
wanao Utamaduni wao? Ndiyo wanao katika nyanja tofauti.Wanao utamaduni wa mavazi,vyakula,maamkuzi na kuvumiliana.Unawezaje kumtafautisha Mtanazania na Mkenya
au Msudani kiutamaduni?Wakati tukichangamsha bongo,wakati wa sherehe za Muungano
kule uwanja wa Uhuru na alasir katika viwanja vya Ikulu tumeshudia ukuu wa Utamaduni wa
Tanzania uliotukuka.Siyo jambo la kawaida kwa nchi changa na hasa za Kiafrika kuonesha uungwana na ustaarabu huo.Mimi nimeona Marais waliostaafu wa Tanzania wakitangulia kuingia uwanjani mapema kabla Rais Kikwete kuingia.Kwa umri hawa wastaafu ni wakubwa
lakini pia alikuwa waziri wao katika vipindi tofauti.Si hivyo ni nadra katika nchi za Afrika kuwaona Marais waliostaafu wanakaa katika safu moja ya Viti huku wakiongea na kucheka.Kwa
mataifa mengine marais waliostaafu hawakutani na hawasemezani.Ukimaliza bila kupinduliwa au kuuwawa ni bahati yako.Rais ambaye hakuwepo ni amekufa kwa kifo cha kawaida. Si mwingine Ila Marehemu Nyerere.Na yenye angekuwa hai labda angehudhuria.Hili la uwanja wa
Uhuru la Marais wastaafu kuwa pamoja na Rais aliye madarakani ni dogo.Huko Ikulu alasiri
kulikuwa na utoaji wa nishani kwa wateule wachache.Ni wengine waliotunukiwa lakini wengine
walikuwa watu wazito.Wakuu wa vyombo na mihimili.Nchi ya Tanzania iliyojenga utamaduni
wa kipekee ndiyo unayoweza kuona maajabu hayo.Wapo Majaji Wakuu wastaafu wa Zanzibar
na Tanzania Bara wamepewa nishani na mmoja Marehemu.Mataifa mengine watu kama hawa
ama Wapo kifungoni au uhamishoni ama hawajulikani walipo.Ni watu waalitoa maamuzi Hata
dhidi Marais wenyewe.Kulikuwepo Makatibu Wakuu Kiongozi si mmoja si wawili.Nao siyo tu
wamekumbukwa ni wazima na afya.Wakuu wa Polisi wastaafu.Nao waalikuwepo na kupewa
nishani zao.Hawa kwa mamlaka waliyonayo walipambana na wahalifu nje na ndani ya serekali.
Lililo gusa nyoyo ni kuwepo na kutunukiwa nishani ni Wakuu wa Jeshi wastaafu mbele ya
Mkuu wa Jeshi aliye madarakani.Wakuu wa Jeshi hao ni Jeneralj Robert Mboma na Jeneral
George Marwa Waitara.Hawa ni watu wakubwa katika Jeshi.Nchi nyingi za Kiafrika watu Kama
labda wangekuwa misutuni wanaongoza uasi,au wangekuwa Marais au wanapigana vikumbo
kutafuta ubunge au wangekuwa marehemu kufatia mapigano ya kusaka madaraka.Sifa za
msingi ya kupewa nishani hizi ni pamoja na ' ...wameonesh maadili mema na kuwa mfano wa
kuigwa hata baadaye ya kutoka madarakani katika kuulinda,kuuenzi na kuuendeleza Muungano'. Kwa vyovyote viwavyo Tanzania imejijengea Utamaduni uliotukuka ambao leo
umeliwekea taifa hili heshima isiyomithilika
J
n
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments