Habari za kuaminika ni kuwa yale mapinduzi yaliyofanyika Burundi yamezimwa. Hatuhitaji kulijadili sana hili linajulikana, na walio bado wakimpinga nkurunziza watayeyuka kidogokidogo mpaka waishe. Ikitokea akaondolewa sasa hayo ni mapinduzi mapya.
Nataka tujiulize kama huyu Jamaa alikuwa kapinduliwa kweli au ni mchezo wa ndani. Na kama alikuwa kapinduliwa amefanikiwaje kurudi?
Mazingira:
Mazingira tuliyomo ni kama tunavyoona. Rais Kagame wa Rwanda anaongoza nje ya muda uliotarajiwa. Rais Kaguta Mu7 wa Uganda naye alibadilisha Katiba ili atawale 'NON STOP". Rais Kabira wa DRC naye yumo kwenye mchakato. Pierre naye amejaribu kubadilisha katiba iliposhindikana akaokota sababu ya kusingizia na inasemekana hata akishindwa lazima atawale la sivyo atarudi maguguni.
Haya katika mazingira haya Nkurunziza angepinduliwa na mapinduzi yakafanikiwa wananchi wa nchi nyingine hizi wangepata somo gani? Je kwa somo hilo Marais hawa wanaweza kuruhusu mapinduzi haya ya Piere yakafanikiwa? Nini itakuwa hatma yao? Bila shaka hawawezi kuruhusu.
Kuna njia kubwa mbili marais hawa wanaweza kufanya au wamefanya:
1) Kuandaa mapinduzi hayo. Hili linawezekana hasa ukiangalia mtu aliyetumika kupindua na jinsi maelezo yalivyokuwa yanaenda. Jamaa alinyang'anywa cheo February. Ametembea kawakusanya waandishi wa habari, kawahutubia na akatumia radio ya mtu binafsi. Ukiangalia unaweza kuyaona kama yalikuwa ill-planned. Sijui hata kama Pierre alikuwa ameisha tua dar Es salaam. Kwa nini apindue sekunde 9 baada ya rais kuondoka? Kwa nini asifanye hvyo kabla hajaondoka? Ni muungwana kiasi gani kutoishusha ndege ilipokuwa ikipaa mambo yakapungua makali? Maana hata ambao walikuja kuzima mapinduzi wasingeshughulika wakati jamaa karest in agony. Kwa hiyo kuna uwezekano kuwa mapinduzi yalipangwa.
2) Lakini njia ya pili ni kuyazima mapinduzi hayo kwa vyovyote vile. Na huenda yamezimwa na marais hawa wanaweza kuwa wameshiriki kwa namna Fulani na kwa sababu zilezile.
Kwa njia zote mbili kuna mabo mawili walitaka yawe:
a) Kumuandaa nkurunziza tofauti na aliyekuwepo. Sasa kila mtu anamuona Nkurunziza kama shujaa wa ajabu. Anaweza kusema wananchi wake wanampenda. Wananchi wale walioshangilia ilipotangazwa kuwa amepinduliwa na ambao walipotea mitaani ilipotangazwa kuwa mapinduzi yamezimwa. Anaweza kusema chochote na ameishasema.
b) Cha pili ni 'sessage sent' kwa raia wa nchi hizi nyingine. Hakuna atakayeweza kuthubutu sasa. Walioingia madarakani kwa nyundo wakikataa kutoka kwa kura lazima njia za ki-kotapin ndizo zinawaweza-sanduku la kura ni kujifurahisha
Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania ameutangazia ulimwengu kuwa nchi za Africa mashariki zitaumaliza mgogoro huu. Tuwape muda tuone.
Elisa Muhingo
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments