M. (Dr.Muhammed Seif Khatib)
Kibafte ni mchezo wa kitoto wa watu wa Unguja.Siyo huo tu, upo mchezo mwingine
uitwao foliti.Upo mchezo wa kitoto uitwao bui.Mwingine huitwa mdako.Orodha ya Michezo ya
kitoto ni mingi sana.Ila sina hakika kama sasa inachezwa humo mitaani na watoto wetu au
wajukuu zetu.Kila mchezo una malengo na dhamira zake mbali Ile ya kuweka akili na mwili
wa watoto katika kuchangamsha na kufurahisha.Hakuna mchezo usio kuwa na somo na
elimu.Yawezekana wachezaji wenyewe kwa maana ya watoto wasijuwe wanachojifunza katika
Michezo.Kwao wao ni mchezo wa kufurahisha tu.Mathalani mchezo wa mdako kama jina lake
linavyosema ni kudaka. Ni mchezo kurusha na kudaka vijiwe.Ni mchezo wa kukaa kitako na
aghlabu mchezo ni wasichana.Ni mchezo ufundishao shabaha ya kudaka vitu na kuimarisha
uwezo wa macho kuona na kuperemba.Bui au kibui Ni mchezo wa watoto wa kufungwa macho
kwa kitambaa na kisha kutakiwa kuwatafuta wenziwe kwa kuwagusa au kupapasa.Mchezo wa
foliti wa kufukuzana mpaka mmoja wao akamatwe.Hata mchezo wa kibafte au kibafute ni
mchezo wa kukisia au kuangalia idadi ya vitu kama punje za nafaka - muhindi au njugu ambazo
zimefumbatwa au kuviringwa katika kiganja cha mkono. Ni kazi ngumu ya kujua idadi ya punje za nafaka zilizomo ndani ya kiganja. Ni siri ya yule anayeweka punje.Kuagua na kutambua ni kazi ngumu sana.Lakini juzi chama kimoja cha siasa kule Zanzibar kimecheza mchezo huo wa
kitoto wa kibafte.La kustaajabisha wachezaji walikuwa watu wazima wenye ndevu,vionjamchuzi
na sharubu.Wachezaji wa chama chenye kuchezesha ni wale wenye wanachama wengi kutoka
Pemba.Anayayetakiwa kuagua ni kutoka chenye wafuasi wengi mikoa ya Bara.Siku hizi wenyewe hujiita UKAWA.Ni mitindo wa kuachiana majimbo. Lakini hakuna jimbo la kuachiana
Ila ni kiini macho tu kwa chama cha Bara.Ama ukitaka kutumia msemo wa mjini ni kumtupia
changa la macho tu.Kuachiana lazima kwanza jimbo liwe lako.Kadhia ni la Kikwajuni mjini
Unguja.Jimbo hili tokea enzi na enzi lilikuwaj la chama cha Afro-Shirazi Party.Hata baada
ya mfumo wa vyama vingi CCM imekuwa ikishinda kila uchaguzi.Hata uchaguzi wa mwaka huu
CCM itashinda.Kusema kuwa jimbo hili ni mbuzi wa kafara wa ukawa ni kuwadanganya
wenzao wa Bara,Kama kweli kuna dhamira ya kweli ya kuachiana majimbo kwa nini mgombea
huyu kwa kumpenda wasimpe Jimbo la hakika la asili la Mji Mmkongwe?Au wakamsafirisha na
kumpeleka huko Pemba kwenye ngome ya chama chao? Atoke Kikwajuni ende Mtambwe
au Wete au Ole.Kama vile hili halitoshi kwa nini isiwe jimbo la Uwakilishi? Kwa nini Urais wa
Zanzibar wawe wao ? Huku hakuna UKAWA?Majimbo yote ya Zanzibar ya Uwakilishi na Ubunge hayamo katika kondoo wa kafara wa Ukawa.Wao wanao msemo wao huku usemao
changu ni changu pekee yangu lakini chako ni chetu sote.Ama chetu ni chetu pekee yetu Lakini
chenu ni chetu sote.UKAWA utawafadia wapinzani wa huku Zanzibar kuliko Bara.
Akina Makaidi na Mbatia hawawezi kuwa wawakilishi,wabunge au Rais wa Zanzibar kwa vile
wao si Wazanzibari.Lakini vyama hi I vinao viongozi huko Zanzibar ambao ni Wazanzibar
kwa nini wasiwape majimbo ya Pemba ili kuonesha mshikamano wa UKAWA?Viongozi wa UKAWA wa vya a yenye mizizi Bara ambao ni Wazanzibari halisi kwa nini wasigombee
Urais wa Zanzibar?Kuachina majimbo nafasi Urais haimo? Kwa nini Urais wa Zanzibar uwe
kwa mtu huyu huyu kwa miaka nenda miaka rudi?Wengine hawana haki? Wengine hawastahiki?
Wengine hawapaswi?Uteuzi wa wagombea waliotajwa juzi na UKAWA wa Zanzibar ni kiinimacho! Ni changa la macho!Ni mchezo wa kitoto uitwao Kibafate! Kilichofumbatwa katika
viganja vya mikono ya wanasiasa hawa hakuna anayejuwa.UKAWA wa visiwani ni kondoo wa kafara! Ni kibafte
K
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments