>
> UTEPETEVU.
> (Dkt.Muhammed Seif Khatib)
> Binadamu ni mja na mahuluku hupata utepetevu.Ni hali ya mwili kuregea na hivyo
> kumfanya mtu kuwa goigoi na mvivu.Utepetevu husababishwa na mambo mengi kubwa katika
> hili ni uchovu uliokithiri.Uchovu ni kule kuwepo kwa hali ya nguvu kupungua mwilini baada ya kazi na shughuli kadha wa kadha kufanyika ambazo humpelekea mtu kuchoka.Lakini wataalamu na matabibu huenda mbele zaidi na kutoa sababu za binadamu kupata uchovu na
> utepetevu.Muda wa kulala usiokuwa na utaratibu husababishwa utepetevu.Unajua mtu mzima
> anatakiwa alale kwa muda gani? Ni kati ya saa nane na tano.Wale mabarubaru muda wa saa
> tisa.Nao watoto wa changa muda wao wa kulala ni saa kumi na sita.Sababu nyingi ya uchovu
> ni utaratibu wa mlo.Mlo usioshibisha husababisha uchovu na hata ukila ukashiba yategemea
> unakula aina gani ya vyakula.Ukiowaona matabibu wa vyakula watakushauri nini ule na nini
> usile kuepuka utepetevu.Mazoezi ya mwili yasipofanyika utavamiwa na utepetevu.Ushauri
> uliopo ni kuwa angalau binadamu afanye mazoezi ya mwili siku nne kwa kila wiki na kila zoezj
> moja lisunguwe muda wa dakika arubaini.Ukosefu wa damu mwilini husababisha uchovu.Hili
> hutokea pale chembe chembe nyekundu katika damu kushindwa kupata oxgin ya kutosha
> na kuisambaza katika viungo muhimu vya mwili.Utepetevu huu huathiri mwili na akili.Umri mkubwa na uzee nao ni sababu ya utepetevu.Nini kinatokea pale utepetevu na uchovu unapomvamia binadamu?Mwili hushindwa kufanya kazi.Hivyo muda wote utalazimika kukaa tu bila kujishughulisha na maisha.Hilo husababisha nishani ya mwili kukosekana.Uchovu mbaya
> zaidi ni wa akili.Hulazimisha muathirika kulala au kusinzia muda wote.Kufikiri na kutoa uamuzi
> huwa na udhaifu mkubwa sana.Wanasiasa nao binadamu.Nao hawawezi kuukimbia utepetevu na uchovu.Kila nafasi ya uongozi ina kiwango cha uchovu.Uchovu wa diwani haulingani na
> ubunge.Uchovu wa Urais si sawa na Mbunge.Kwa Urais aliye madarakani panda shuka na
> hekaheka yake kwa miaka mitaano au kumi mfululizo hatakuwa machovu muda wake ukisha?
> Hata kabla kwisha muda wake atachoka tu.Uzuri wa uchovu wa Urais ni kuwa anautumia muda
> wake kwaajili ya kuwahudumia watu wake na taifa lake.Ni Rais anashughulikia mambo mengi na sekta nyingi wakati watu Wengine hawana habari na yanayotokea nje ya kuta za nyumba yake.Rais wa CCM katika miaka kumi ya uongozi wake katika sekta moja tu ya barabara amefanya mengi.Tanzania inao mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometers 35,000 ambazo zinajumuisha kilometers 12,786 za barabara kuu na kilometers 22,214 za barabara za mikoa.Katika muda wa uhai wa uongozi wake jumla ya kilo its 13,753 zimeshighulikiwa kwa
> viwango tofauti.Barabara zen ye urefu wa kilometa 4,691 zimekamilika kujengwa kwa lami.
> Barabara nyingine zenye urefu wa kilomita 2,358 hivi sasa zinaendelea kujengwa kwa kiwango
> cha lami.Aidha barabara nyingine zenye urefu wa kilomita 3,419 zimefanyiwa upembuzi na usanifu kwaajili ya ujenzi.Hivi kazi hiyo ndogo?Lakini ieleweke mafanikio hayo ni ya sekta moja tu.Mengi yamefanyika katika sekta nyingi za uzalishaji,ulinzi,u humo,jamii na miundombinu ambazo kuziona hazihitaji darbuni wala hadubin!Bila ya shaka jitihada zake na wasaidizi wake
> ndiyo zizaazo matunda makubwa ya maendeleo.Kama binadamu kazi pevu na ngumu lazima
> itamchosha.Lakini kwa sababu chama choke ni kikomavu kitamwandalia Kiongozi mwingine
> wa kumkabidhi kijiti cha uongozi wa Urais.Lakini uchovu na utepetevu huwapata hata wale
> wautakao urais wa kambi ya upinzani.Wanaupata vipi? Mfumo wa vyama vingi katika uchaguzi
> wa Urais ulikuwa mwaka 1995.Rais Mkapa alianza kukimbiza kijiti cha Urais.Unawakumbuka
> wale aloshindana nao wakati huo?Mwangaliye Rais Mkapa wa mwaka 1995 na leo kwa sura
> wajihi na haiba!Watazame wale aloshindana nao! Mzee 'Mapesa' na 'Mzee Kibandiko',Zitizame
> sura zao,mili yao na jinsi wanavyotembea.Si 'majeneza' yanayotembea?Mtazame Maalim yule
> aliyeutaka Urais na kushindana na Marais wa nne katika vipindi tofauti.Ni zaidi ya miaka thalathini na tano anahaha kusaka Urais kwa ticketi ya upinzani.Alishindana na Mzee Wakili,
> Rais Salmin Amour,Rais Amani Karume na Rais Shein.Mtazame Maalim alivyo leo kiafya,
> sura yake,wajihi wake,haiba yake na anavyotembea.Kuna mtu?Wale aloshindana nao kwa
> vipindi tofauti wapo wapi leo? Rais Wakili amefariki,Rais Salmin amestaafu,Rais Amani Karume
> amestaafu na Dr.Shein anamsubiri mwezi Oktoba mwaka huu.Hivi Maalim katika mazingara
> haya bado Hana utepetevu na uchovu?Kama 'Mzee wa Mapesa" amechoka,'Mzee wa Kibandiko' amechoka - na wote wamebwaga manyanga, Maalim anasubiri nini?
>
>
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments