[wanabidii] Fwd: Vitalu

Sunday, April 19, 2015


Sent 
Subject: Fwd: Vitalu



Sent from my iPad

Begin 

Subject: Vitalu

                                                             Vitalu
                                (Dkt.Muhammed Seif Khatib)

             Maumbile yameigawa nchi katika maeneo tofauti.Yapo maeneo yenye ujazo wa maji.
Nayo maji yapo ya chumvi huitwa bahari.Viumbe vyake vyaweza kuishi humu kwa miaka bila
kudhuriwa na wingi wa chumvi iliyomo.Viumbe viliyomo hupata riziki zao kwa vyanzo na nyenzo tofauti.Wengine hulana wenyewe kwa wenyewe.Siyo maji ya chumvi tu hata maji
yasiyo na chumvi yaitwayo maziwa na mito ndani yake huishi viumbe.Ipo ardhi,nchi kavu.
Miji, mitaa, vijiji na vitongoje huwepo nanimatokeo ya akili na ujuzi wa binadamu.Ardhi huwa na watu na wanyama.Ili kuishi na kujiletea maendeleo,watu hufanya kazi na kuendeleza miji
yao kwa kujenga nyumba,miundo mbinu na harakati kadhaa. Maisha yao hurefuka na kuwa
na afya kwa sababu kwa kufanya kazi hupata fedha za kuweza kununua chakula na kunipatia riziki zao.Miji na mitaa pamoja na vitongoji huwa chini ya miliki ya binadamu.Eneo la tatu la ardhini ni pori au wengine huita misitu.Eneo hili hushonana kwa miti ya kila aina kwa miaka nenda miaka rudi.Miti haikupandwa na binadamu bali imejiotea wenyewe.Katika
pori ni makaazi ya wanyama wakubwa na wadogo.Ni mkaazi ya ndege na wanyama.Humu maisha ya viumbe hutegemea mimea,matunda,maua,mizizi na kulana viumbe hao wenyew
kwa wenyewe.Pori si makaazi ya binadamu ingawa binadamu ni mtawala wa dunia na vyote
viliomo.Ni yeye anayevua vilivyo baharini.Ni yeye anayevuna vilivyo ardhini .Ni yeye pia
anayewinda vilivyo porini.Uwindaji wa wanyama katika pori hugawiwa katika maeneo
yaitwayo vitalu.Humu ndimo mwenye nyara.Uwindaji huwa kwa kuua tembo ili pembe zake
zilete utajiri.Vifaru huuliwa kwaajili ya pembe zake. Simba,chui na punda milia huuliwa kwaajili ya kuchunwa ngozi zao.Nyara hizo huwa ni mali na utajiri kwa mwanadamu lakini ni
mauti na majanga kwa wanyama wenyewe..Wanasiasa umefika msimu wao sasa kugawana vitalu.Ni vitalu vya kuwindia wanyama pori.Nchi itagawiwa  katika majimbo saw
na  vitalu vya wanyama.Vipo vitalu vyenye wanyama wengi wenye kupendwa na wawindaji  ambao nyara zao zina soko.Watu kadha sasa wanajiandaa kutafuta kwa udi na uvumba
vitalu.Watu hujinasibu na kujinata kuwa sasa wameamua wende katika maeneo ya kwao
walipizaliwa, kwenye vitalu vya asili,ili 'kuwasaidia' na kuwatoa katika 'umasikini' watu wao.Katika kipindi  hiki kila mtu anakujua kwao.Katika majira haya watu ndiyo wanakumbuka kwao.?Msaada wa kuwapa watu wa kwao ni kipindi hiki?.Shida na dhiki  za
watu wa kwao wanazijua wakati huu? Umasikini wa watu umejitokeza  wakati huu?Lakini
wanaokujua kuwa sasa wapo watu wa kwao si kutoka chama kimoja tu.Vyama utitiri vyote
vitatatoa 'wawindaji' wenye huruma na kwao.Kama si kwa sheria inayokataza mtu binafsi
kugombea, basi idadi ya 'wawindaji'ingekuwa wengi. Vitalu vya wanyama vingevamiwa na
na kila mtu.Wengi ya watu hawa hawapiti huko makwao.Wapo waliohama tokea utoto na
ujana na kulowea mijini katika majiji.Hawendi kwao, si wakati wa Eid au Krisimasi au mwaka mpya.Hawashiriki sherehe za jando au unyago. Hawashiriki vipaji mara au Maulid.
.Hawendi harusini hawendi mazikoni.Huku kwao hawana nyumba hawana vibanda.
Wengine hata wazee wao wamewatelekeza.Wanachoendea ni kupata 'nyara' na wingi wa
 'vitalu'  vizuri..Wapo wanaokwenda kwao baada ya kustaafu kazi.Wachovu hawa huwa
wanajikongoja  kuelekea majimboni kutafuta masilahi..Ukimwuliza amewafanyia nini watu
wa kwao alipokuwa anafanya kazi? Jibu ni hana  alofanya.Wapo wengine wanaokwenda kugombea baada ya kufukuzwa kazi.Huko hutafuta 'ajira' katika vitalu vilivyoshiba
nyara. Makundi yote hayo yataelekea mijini,vijijini na vitongojini kuwinda katika 'vitalu'.
Bila ya shaka katika harakati za uwindaji mbugani athari zitatokea.Wawindaji kwa
wawindaji wanaweza wao wenyewe wakajeruhiana.Ama yawezekana wawindwa hasa
wanyama wakali wakawajeruhi wawindaji na hivyo  kutimua mbio mbugani ili kunusuru
roho zao.Vitalu vina gharama yake kwa wawindwa na wawindaji.Wale wanaofanikiwa
kupata vitalu vyenye wanyama wenye thamani viungo vyao hufurahia mawindo yao.Wengi wao wakifanikiwa kupata 'nyara' huku wakiwaacha wanyama na majaraha na 'mizoga 'ya
miili yao huwa hawarudi tena mbugani na  huwa mbali na 'vitalu  hadi msimu mwingine baada
miaka mitano.Hawapiti mbugani na katika ' vitalu' kujua mahitji ya wanyama,ndege na wadudu wa mbugani.Wawindaji walilolijia wamelipata.Hufaidika na utajiri wa ' nyara' za
kutoka vitaluni ni ile ahadi yao ya kurudi kwao ili kuwasaidia watu wao wa kuondoa umasikini huwa haikumbukwi tena.Wawindaji hao baada ya kukusanya nyara hawapiti
vitaluni hadi baada ya miaka mitano ipite. Watarudi kuingia mbugani na kuomba kibali cha
kuwinda katika 'vitalu'. Wenye 'vitalu' mbugani tahadharini na wasasi wasakao 'nyara'
zenu!



Sent from my iPad

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments