> Karume
> (Dkt.Muhammed Seif Khatib)
> " ...ikapigwa risasi kutoka mlangoni; ikampiga Mheshimiwa Sheikh Karume shingoni.
> Hapo hapo akaanguka...wakati huo huo risasi ikanipiga mimi katika sehemu ya mkono,
> nikaanguka upande wa kushoto...ikawa nimeviringika chini ya meza." Sheikh Thabiti
> Kombo anasimulia yaliyojiri tarehe 07.04.72 hapo Kisiwa Nduwi saa 11.45 magharibi.
> " Kijana alotupiga risasi alikuwa anaitwa Humud, kijana wa Kiarabu aliyekuwa na cheo
> cha Luteni katika jeshi"Sheikh Thabiti akimtaja mtu aliyemwua Karume na kumjeruhi yeye.
> Nani aliyewahi kufika kwa haraka katika tukuio hilo? Ni Ali."Ali Mahfudh akaniangalia kwa
> makini apate kujua kama nimekwisha malizika au bado..."Jee ,Ali,mbona hivi;nchi imekwisha pinduliwa?"Sheikh Thabiti aliuliza! Sheikh Thabiti akasema; " Mimi nilipata maumivu makubwa sana , risasi nyingi ziliniingia mwilini na kusababisha viungo vyangu kupata ulemavu.Lakini mimi si kitu.Maumivu makubwa tuliyoyapata Afro-Shirazi kumpoteza
> Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Karume"(Mdundo.1969.DUP)
> Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 04.08.05 huko Mwera, Unguja aliuliwa kikatili
> mbele ya wazee wenzake na hakuwa na kinga yeyote. " Wakati zilikuwa zinakuja risasi
> nilikuwa nikiona zinampiga Karume katika ubavu wa kushoto,'siwezi kujua yeye
> alipigwa risasi ngapi ...ukiacha ile iliyomvunjs shingo"(Mdundo.1969.DUP). Naye Thabiti Kombo alipigwaje risasi? " "Mimi nilipigwa risasi tatu mguuni ; ya kwanza ikanivunja mfupa,ya pili katika goti,na ya tatu pajani mguu,wa kushoto.Risasi nyingine ilinipiga katika gungu la kiuno kuingia takoni"(Mdundo.1969.DUP).Unyama gani huu kuuwa na kujeruhi?
> Karume aliyeshiriki kuunda chama cha Waafrika wa Zanzibar na mwenzake
> Thabiti Kombo hawastahiki adhabu hiyo.Chama walichokiunda tarehe 05.02.57
> kiliundwa kumkomboa Mwaafrika dhidi ya utawala wa Kisultan uliodumu Zanzibar tokea
> mwaka 1832 hadi Januari 12.1964. Wakati Waafrika wanakiona chama hiki ni cha ukombozi viongozi wa vyama vya kihafidhina kama HIZIBU wanakinyanyapaa na kuona kuwepo kwake ni balaa.Kiongozi wa HIZIBU Sheikh Ali Muhsin Barwani anakionaje? Ni kitendo kiovu cha kuundwa ASP kilicho tokea katika mwaka 1957 ni maafa makuu.".Miaka saba ya vuta nikuvute ya harakati za siasa dhidi vyama vitatu vya
> siasa vya Hizbu,ZPPP na Umma Party kwa upande mmoja na kwa upande wa pili ni
> Serekali ya Mwingereza na Sultan ni kipindi cha mapambano makali.Waafrika wa Zanzibar waliamua na kudhamiria kukata minyororo ya utumwa na utwana.Walishikamana
> kuukataa ukoloni wa Kingereza na Usultani wa Kiarabu.Walipigania washike dola yao
> iliyopokonywa kwa ubia wa Mwengereza na Sultan.Walitaka wadhibiti ardhi yao yenye
> rutuba walionyanganywa kwa zaidi ya karne moja.Badala ya Waafrika wa Zanzibar
> kuwa vibarua,manamba na manoko wa mashamba ya watu wachache, walitaka sasa
> wao iwe mali yao.Ni ardhi yao ya asili walioporwa na walowezi.Waafrika wa Zanzibar
> waliogeuzwa wachukuzi na makuli, sasa walitaka washike hatamu za kiuchumi za
> uchumi wa Zanzibar.Walipigana kufa kupona ili hatamu za kiutawala ziwe mikononi
> mwa Waafrika.Muhimili wa Mahakama uliokuwa unaongozwa na kikundi kidogo cha
> wageni ulipaswa irudi mikono katika ya miliki ya wenyeji waliwengi.Hivi dhamira
> hizi zenye lengo la kunufaisha wengi ni za kuwajengea uwadui viongozi wakuu wa Waafrika
> chini ya chama cha ukombozi cha Afro-Shirazi Party? Waafrika wa Zanzibar kike kwa
> kiume walishikamana.Hawakuwa na mali wala elimu.Hawakuwa na uzoefu wa siasa.
> Hawakuwa na ajira serekalini.Ni watarazaki na wachuuziu.Ni wakwezi wa minazi na
> wachumaji karafuu.Ni wavuvi na wachungaji.Ni wachukuzi sokoni na makuli bandarini.Ni
> washona cherehani na fundi wa baiskeli.Ni maboi na matopasi.Tabaka hili nyonge na dhaifu
> lilipigana kufa kupona dhidi ya vyama vya wasomi, wenye mali na waajiiriwa serekalini.
> Vyama vya upinzani dhidi ya Afro-Shirazi viliungwa mkono na mabwanyenye wa Kiarabu
> na Wafanyabiashara wa Kihindi.Sultni wa Kirabu hawakujificha kuonesha upendeleo
> wao kwa vyama vya Hizbu na ZPPP.Njama,ghilba na usaliti wao badala ya kuwogofya
> wanachama wa Afro-Shirazi Party uliwapa nguvu na ari.Uchaguzi ukipangwa,
> Afro-Shirazi huongoza.Hata hivyo kwa njama za Mwingereza kwa kushirikiana na
> Sultan wa Kiarabu wakawabeba ZPPP na HIZIBU(Z.N.P) ili wawape serekali.Kuwapa
> Serekali wao ni kumlinda na kumbakisha Sultan milele.Tarehe 9 Disemba 1963
> "UHURU" wa bandia ukasherehekewa Zanzibar na watu wachache.Waafrika wengi
> wakasononeshwa kwa kunyimwa dola Waafrika wa Zanzibar.Hata hivyo, sauti ya wengi
> ni sauti ya Mungu.Wengine husema; ' Wengi wape,usipowapa watachukuwa kwa mikono
> Yao".Januari 12 mwaka 1964, Waafrika wa Zanzibar wenye hasira wakamua kuipindua serekali na kumtimua Sultan Kiarabu.Sheikh Ali Muhsin wa HIZIBU akawarejesha
> wapenzi wake kulaumu Afro-Shirazi chini ya Abeid Karume kwa kufanikisha Mapinduzi
> Matukufu kwa kudai," Hii ASP ndiyo ilosababisha kutenda maafa(Mapinduzi) Januari 12
> mwaka 1964(Barwani,2003, Oman).Wakati tupo na kumbukumbu ya kuomboleza kwa kuuwawa Abeid Karume, maneno ya mashirika wake mkuu,Marehemu Thabiti Kombo
> yanatupa faraja Waafrika wa Zanzibar pale aliposema;
> "Mafisadi walidhani kuwa akiuwawa Karume basi mapinduzi yatakoma.Karume kweli
> amekufa, amezikwa lakini mapinduzi yamebaki mpaka leo".
>
>
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments