[wanabidii] FM ACADEMIA WANAREKODI NYIMBO MPYA

Monday, April 20, 2015

FM ACADEMIA WANAREKODI NYIMBO MPYA

Na Happiness Katabazi
BENDI ya FM Academia (Wazee wa Ngwasuma) ,hivi sasa wapo Studio wanarekodi nyimbo mpya .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mhasibu wa bendi hiyo Calvin Mkinga alisema nyimbo ambazo zimeanza kurekodiwa ni wimbo wa Watabiri uliotungwa na Mulemule FBI na Bodaboda Kariakoo ulitungwa na Kingombe Blaise'Kingblaise' na kwamba wanarekodi nyimbo hizo katika studio ya Metro, watunzi wa nyimbo hizo ni hapo pichani.

Pichani kushoto ni Mulemule FBI na ( kulia),Kingblaise.
Mkinga alisema Redio na Televisheni zimetoa masharti kwa bendi za muziki wa dansi nchini kuwa ili ziwe zinapiga nyimbo za bendi za muziku wa dansi ni lazima bendi hizo zitunge nyimbo zitakazoimbwa kwa dakika chache kwani mifumo ya utangazaji iliyofungwa katika vituo vya redio na Televisheni ni mfumo wa kisasa ambao hautaki kupiga wimbo wenye dakika nyingi,unaitaji wimbo uwe ni wa dakika nne tu.

' Wanamuziki wetu walizoea kutunga wimbo unaopigwa kwa dakika 15 sasa hivi sharti linataka watunge nyimbo zenye dakika nne na tayari wanamuziki wetu wameishatunga nyimbo kadhaa nazimeishaanza kurekodiwa na kwamba jumla wanatarajia kurekodi jumla ya nyimbo sita.alisema Mkinga.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Aprili 20 mwaka 2015.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments