> SUSA.
> (Dkt.Muhammed Seif Khatib)
> Waswahili wanalo neno lenye herufi nne tu lisemalo 'SUSA'.Ingawa neno
> hili lina maana zaidi ya moja lakini katika muktadha wa jambo tunalojadili
> maana mjarabu ni ;ni kule kuacha kufanya jambo kwa sababu ya kuchukia au
> kutoridhiswa na jambo linaloendelea au mwelekeo wake.Uamuzi wa kususa
> unapelekea kuacha kushirikiana au kuwa na uhusiano kabisa.Mwaka 1992 chama cha Mapinduzi kilirasimisha watu wapendao kuanzisha vyama vya siasa
> wafanye hivyo.Uamuzi huo ulifanywa na Halmashauri Kuu ya Chama cha
> Mapinduzi.Mwalimu Nyerere alishiriki katika uamuzi huo mgumu.Chama kikamtaka yeye
> mwenyewe atoke hadharani na ' kupasua mbarika'.Bila kumunyamunya maneno,Mwalimu akaelezea jambo hilo kwa ufasaha na kutaka yeyote yule
> atakaye aunde chama na jambo hilo si kosa tena.Taratibu za kisheria na kibunge
> zikafatwa na uchaguzi wa kwanza ukafanyika katika uchaguzi mdogo wa
> Kwahani, huko Zanzibar wa Ubunge mwaka 1992. Tokea mwaka huo ambapo
> Mwalimu yupo hai hadi leo mwaka 2015 imetima miaka ishirini na tatu, vyama
> vya siasa vimekuwa vikuundwa. Ukiacha Chama Cha Mapinduzi kilichozaliwa
> upya katika mikono ya Nyerere na kupata baraka zake vyama vyengine
> ishirini na moja viliundwa na kuimarishwa.Ingawa Chama Cha Mapinduzi ndiyo
> chenye kushika hatamu hakijaweka mkono wake kuzuia kuzaliwa kwa vyama
> vipya.Vyama kadha vya upinzani dhidi ya Chama Cha Mapinduzi vikaruhusiwa
> hadi kufika vyama vyote ishirini na mbili.Unavijua vyama hivi na lini vimezaliwa? CCM (1977);CUF(1992); CHDEMA(1992); UMD(1993);
> NCCR(1992);NLD(1993);DEMOKRASIA MAKINI (2001); UPDP (1993);
> NRA(1993);DP (2002);TADEA(1990);TLP (1993);UDP (1994);
> CHUSTA (1998);PPT MAENDELEO (2003);SAU(2005), JAHAZI
> ASILIA (2004);AFP(2009);CCK (2012);ADC (2012);CHAUMA
> (2013) na ACT (2014). Tunajifunza nini kwa ujio wa vyama vyote hivyo? Kwanza Nyerere alibariki kuwepo kwa upinzani lakini yeye hakuunda chama upinzani dhidi ya
> Chama Cha Mapinduzi.Angetaka angefanya hivyo.Yeye akikipenda na kukiamini kuwa
> ni chama bora.Kauli zake kadha zikithibitishwa mahaba yake juu ya chama hiki.Kauli
> isemayo,' Bila CCM imara nchi (Tanzania) itayumba'.Mwalimu alikuwa akitoa ushauri
> na maelekezo kwa chama chake kuwa kunapaswa kuimarishwa ili Taifa la Tanznia lisije
> likasambaratika.Hakuvitaja vyama vyengine ambavyo tayari vilikuwa vimeshaundwa.
> Kauli nyingine ya Mwalimu aliyoitoa kuwambia Watanzana juu ya umakini na umahiri wa
> Chama cha Mapinduzi akihusisha Urais mzuri atatoka ndani ya chama chake na si kutoka
> vyama vyengine viliopo na vile vitakavyokuja.Alisemje? ' Rais wa Tanzania anaweza
> kutoka Chama Chochote lakini Rais Bora atatoka ndani ya CCM'.Mifano miwili hii
> ni bayana kuwa Mwalimu alikuwa Mwana CCM kindakindaki na hakutetereka hata
> mara moja tofauti na baadhi ya wanaojaribu kuonesha kuwa mwalimu alikisusia Chama Cha Mapinduzi.Mwalimu ameishi miaka saba baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama
> vingi.Alifariki dunia huko London tarehe 14 Oktoba mwaka 1999 pale alipolazwa hospital kwa maradhi ya 'leukemia' na kuzikwa kijijini kwake Butiama tarehe 23 Oktoba.Mwalimu
> hakususia Chama cha Mapinduzi. Yeye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ya
> kudumu hata baada ya kung'atuka.Mwalimu alishiriki kikamilifu katika mchakato wa
> kumtafuta Rais Bora kutoka ndani ya CCM katika uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi
> mwaka 1995.Alishiriki katika Mkutano Mkuu wa kumteua mgombea wa Urais kutoka
> chama chake.Kama vile haitoshi yeye mwenyewe kwa hiyari yake alizunguka nchi nzima peke yake kila mkoa huku akimpigia debe la kutosha Benjamin Mkapa kuwa ndiye Rais
> atakayewafaa.Aliwatahadharisha Watanzania kuwa wasiwachaguwe wagombe wa
> Urais kutoka vyama vya Upinzani vya CHADEMA, UMD,CUF na NCCR.Naam!
> Watanzania wakamsikiliza Mwalimu, wakamwelewa na wakamchaguwa Rais bora
> kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi.Hakuwa mwengine isipokuwa Benjamin Mkapa.
> Watanzania hata baada ya kufa Mwalimu, mwaka mmoja baadaye waliendelea kufata
> wasia wake na kumpigia kura Benjamin Mkapa.Lakini tunaona kuwa baada ya kuundwa
> chama cha upinzani cha CHADEMA au CUF ama NCCR ingetarajiwa kuwa viongozi wa
> vyama hivi wangekisusia Chama cha Mapinduzi tu na kuunda chama kimoja tu dhidi ya
> CCM.Kinyume chake viongozi wa upinzani siyo tu wamekiasi na kukisusia Chama Cha
> Mapinduzi tu lakini wao wenyewe kwa wenyewe wamekuwa hawaaminiani.Kila chama
> kinachoundwa ni ushahidi kuwa wanawasusia wapinzani wenzao na kujitenga nao. Chama
> cha upinzani kilianza kimoja mwaka 1992 lakini leo vipo ishirini na moja. Huu ni ushahidi kuwa kila chama kikiundwa maana yake viliopo havina maana na vinasusiwa.Sidhani
> kama vyama vipya vya upinzani vyengine haviundwi sasa.Lazima vitakuwepo.Navyo
> vitasusiwa na wapinzani wenzao tofauti ni Chama Cha Mapinduzi hakijasusiwa na Mwlimu
> kinyume chake kimepata baraka na radhi zake!
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments