Ninaamini kabisa kuwa Zitto Kabwe alikosea na makosa mengine ni makubwa, na makosa hayo yamemfikisha hapa alipofika.
Ninaamini pia kuwa Zito amevunja taratibu za chama chake na ni sababu tosha za kumchukulia hatua alizochukuliwa na chama chake.
Ninaamini pia kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimekosea kisiasa kumchukulia hatua kilichoichukua.
Sijui kama Zitto alifanya makusudi kosa hili la mwisho (kupeleka CDM mahakamani) Nasema hivyo kwa sababu anaweza kuwa alijua kosa kitakalofanya chama akaamua kufanya hivyo ili kikosee.
Sijui kama CDM ilipima nini inaweza kuwa athari za kumfukuza uanachama Zitto.
Ninajua pia kuwa Chadema imemjenga zaidi Zitto zamu hii (kwa kumfukuza) kuliko huko nyuma. Namna alivyofanya kujitoa bungeni imemjengea jina kuliko makosa yake yalivyombomoa.
Kwa hiyo najua pia kuwa CDM inaweza kujeruhika kwa kutonyamaza baada ya uamuzi wa mahakama. Harakaharaka hiyo haikuwa na mbaraka
Kwa makusudi ya umoja na ustawi wa Taifa hili natamani Zitto afanye moja kati ya mambo haya mawili:
Ajiunge na CCM AU
Abaki ndani ya UKAWA kwa kujiunga na moja kati ya vyama wanachama. Hii itaendeleza nguvu yake na itamjenga Zitto zaidi. Si muda mrefu atakuwa karibu na chama anachokipenda CDM.
Asipofanya hivyo najua kuwa atarudi Bungeni kupitia chama kingine (huenda ACT) lakini matarajio yake hayawezi kutimia akiwa huko. Hataweza kujirekebisha huko kwa sababu dhambi iliyowatoa CDM itaivuruga ACT siku moja.
Mwisho natamani kujua kama Zitto amesoma ujumbe huu. Mimi sionekani (ni mtu mdogo kisiasa) japo nadhani mawazo haya yanaonekana.
Elisa Muhingo
0767187507
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments