[wanabidii] ZITTO KABWE ANUIA KUJIONDOA BUNGENI MAPEMA

Thursday, March 19, 2015

Mbunge wa kigoma kaskazini Zitto Kabwe amefanya mazungumzo ya faragha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano Anne Makinda hapo jana kwenye kikao kilicholenga kujadili na spika iwapo ajiondoe mapema kwenye ubunge ama laa

Gazeti la serikali limechapisha hivi leo taarifa hiyo ambayo pia imearifu kuwa zitto amekutana vilevile na Spika wa zamani Samwel Sitta kushauriana naye juu ya suala hilo la hatma ya ubunge wake.

Kulingana na taarifa zilizopo ambazo hata hivyo hazikuthibitishwa na upande wowote, zitto ananuwia kutangaza kujiondoa bungeni mapema kabla ya hatua za kusubiri barua ya chama chake kumfikia spika wa bunge na kisha kiongozi huyo kuiarifu tume ya uchaguzi juu ya uamuzi wa Chadema wa kumvua uanachama ili chombo hicho kitangaze kuwa jimbo hilo liko wazi.

Hatua hiyo ya mbunge huyo mashuhuri kufanya mashauriano na spika wa bunge na kiongozi wa zamani wa chombo hicho ni ya karibuni kabisa tangu chadema itangaze wiki moja iliyopita kuwa ubunge wa Zitto umekoma kutokana na matakwa ya katiba yanayoainisha mwanachama atakaeshindwa kesi mahakamani dhidi ya chadema atakua amejiondoa chamani.

Aidha taarifa ya makutano hayo ya Zitto na viongozi wa juu wa bunge yanakuja wakati mbunge huyo ametangaza mwishoni mwa juma la jana kwamba hatowania tena kipindi kingine cha ubunge kwenye jimbo la kigoma kaskazini alilohudumu kwa muongo mmoja.

Una maoni gani?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments