YALIYOMKUTA KIDEKU NA UNGO PIA YATAMKUTA. Na Happiness Katabazi YAANI NAMAANISHA YALIYOWAHIKUWAKUTA WANASIASA WENZAKE PRO.SOSPETER MUHONGO,PRO.ANNA TIBAIJUKA,ANDREW CHENGE, ALIYEKUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ,JAJI FREDRICK WEREMA ,ELICHIM MASWI NA WENGINE WENGI PIA LEO NAE BINGWA WA KUPENDAGA SANA KUSHINIKIZA WANASIASA WENZAKE WATKMULIWE KAZI NA WAJIUZULU NYADHIFA ZAO YAANI ZITTO KABWE NAYE YAMEMKUTA AMETANGAZA RASMI KUJIUZULU UBUNGE NDANI YA BUNGE USIKU HUU. LICHA ZITTO YEYE KAPATA MAPIGO MFULULIZO KAMA KUSHINDWA KESI YAKE MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM,,KUFUKUZWA UANACHAMA,KUJIUZULU UBUNGE NA KUPOTEZA NAFASI YA UENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA PAC.MUHONGO ,TIBAIJUKA YEYE KAPOTEZA UWAZIRI,UJUMBE WA KAMATI KUU (CCM)WA TIBAIJUKA,NA CHENGE NA NGELEJA WAMEPOTEZA NAFASI YA UJUMBE WA NEC.NA ZILE FEDHA ZA ESCROW TIBAIJUKA,CHENGE,NGELEJA WANAZO HAWAJANYANGANYWA NA BADO WANAENDELEA KUWA WABUNGE. ILA ZITTO VYOTE KAPOTEZA KWA KIPINDI KIFUPI SANA.POLE ZIT TO HIYO NI AJALI YA KISIASA NA PIA MUNGU ANA SABABU YA KURUHUSU MACHUNGU HAYO YAKUFIKE.ALIKUWA NA UWEZO WA KUZUIA YAKUFIKE. .NAKUSHAURI TULIA ,ACHA KUONGEA ONGEA SANA NA MEDIA UTAFAKARI.MUNGU ALIKUWA NA UWEZO WA KUZUIA HAYO MAPITO HAYO USIYAPOTE LAKINI YEYE KARUHUSU YAKUFIKE. UENDA ANA SABABU ZAKE AMBAZO HUZIJUI.PIGA GOTI NAMSHUKURU MUNGU KWA YOTE HAYO.NAAMINI HUKUPENDA UACHIE UBUNGE AU UFUKUZWE CHADEMA ILA UNAJIKAZA KIUME. POLE SANA ILA KAA PEKE YAKO UMUOMBE MUNGU AKUONYESHE ULIKOSEA WAPI?JE HAYO YALIYOKUKUTA NI KISASI CHA MUNGU KWA NIABA YA BAADHI YA WANASIASA WENZAKO NA WATENDAJI WA SERIKALI KUWA WAKATI ULIPOKUEA MWENYEKITI WA PAC,ULIWAUMIZA BILA HATIA? JE ZITTO AJIULIZE KI MOYO MOYO WAKATI ANATENDA MAJUKUMU YAKE AKIWA NA NYADHIFA ZILE ALIKUWA AKITENDA KWA HAKI MUDA WOTE? JE ALIKUWA MSAFI? NAKUSHAURI USILIPE KISASI.KUWA MAKINI SANA NA BAADHI YA WANASIASA WENZAKO AMBAO LEO HII WANAJIFANYA WANAKUONEA HURUMA NA KUJIFANYA WANATUMIA UAMUZI WA CHADEMA KAMA NGAZI YA KUJIPATIA UMAARUFU,WANAFKI NI WENGI. TAMBUA KIPATO,AJIRA SIYO NI KUPATA MADARAKA YA KIBUNGE KAMA UNAVYOFIKIRI,AJIRA NI KOKOTE. JANA WAKATI UNAAGA BUNGENI ULISEMA MUNGU AKIPENDA UTAWEZA KUWA KATIKA BUNGE JIPYA LA NOVEMBA NA MAPEMA WIKI HII UMENUKULIWA UKISEMA KUWA IPO SIKU UTAKUJA KUWA KIONGOZI MKUBWA KATIKA TAIFA HILI NA UKASEMA PIA WANAOKUTABIRIA KIFO CHA KISIASA WASUBIRI KIDOGO. HIZO NI NDOTO ZAKO SIKUINGILI.ILA NAKUSHAURI ZITTO NENDA KAFANYEKAZI ZA KITAALUMA KWA MUDA KADHAA ,MIAKA KUMI NI MINGI . JIFUNZE KWA WAZIRI NA MBUNGE WA MUDA MREFU JOHN MALECELA,JOSEPH MUNGAI WALIOTOKA KWA AIBU YA KUSHINDWA KATIKA UCHAGUZI WA UBUNGE MWAKA 2010 NA MUNGAI AKAISHIA KUFUNGULIWA KESI YA RUSHWA IKAMSUMBUA LAKINI BAADAE MAHAKAMA IKAMFUTIA KESI. NAAMINI SASA UKIREJEA MAKALA ZANGU TATU ZA MIAKA YA NYUMA ZILIZOKUWA NA KICHWA CHA HABARI, (Zitto Kabwe mbona umsahaulifu), (Zitto Kabwe unajiandalia anguko) ,(Kashfa ya Escrwo isitugawe), (Zitto Kabwe ndio ujue sasa muosha uwoshwa tena wakati wa kuoshwa ulipuliwa). Na ile makala ya Mwandishi wa habari mwandamizi,Absalom Kibanda iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho (Naliona anguko la Zitto). NILIYOKUWA NAKUTABIRIA KATIKA MAKALA HIZO YAMETIMIA. TAMKO LA ZITTO HILO HAPO CHINI AMELITOA USIKU HUU BUNGENI.By Happiness Katabazi,Machi 20 mwaka 2015 Facebook:Happy Katabazi Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com 0716 774494 |
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments