TAASISI ya wa Mashekhe na Wanazuoni Kiislamu nchini, wameiomba Serikali kupuuza tamko lililotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) badala yake iendelee na mchakato wa Mahakama ya Kadhi na Maaskofu wawe wavumilivu kwani Serikali ni ya Watanzania wote.
Aidha, imewasisitiza Watanzania kwa ujumla wao kupata elimu ya Katiba Inayopendekezwa na kuisoma kwa makini na kuielewa vilivyo ili wawe na uwezo na uhuru wa kuchagua kile wanachokiona kina manufaa kwao bila kuwepo shinikizo la kiimani.
Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Shekhe Khamis Mataka aliyasema hayo leo jijii Dar es Salaam wakati akitoa tamko la taasisi hiyo kufuatia tamko la TCF kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Mahakama ya Kadhi na Hali ya Usalama na Amani ya Nchi.
Alisema.
-- Aidha, imewasisitiza Watanzania kwa ujumla wao kupata elimu ya Katiba Inayopendekezwa na kuisoma kwa makini na kuielewa vilivyo ili wawe na uwezo na uhuru wa kuchagua kile wanachokiona kina manufaa kwao bila kuwepo shinikizo la kiimani.
Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Shekhe Khamis Mataka aliyasema hayo leo jijii Dar es Salaam wakati akitoa tamko la taasisi hiyo kufuatia tamko la TCF kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Mahakama ya Kadhi na Hali ya Usalama na Amani ya Nchi.
"Taasisi imezipitia kwa kina nukta zote nne za Tamko hilo pamoja na hitimisho lake na kubaini kwamba maaskofu wamejisahau kwamba wao ni viongozi wa kiimani na kiroho ambao wanatakiwa wawe tayari kumpokea yeyote na kumpa neno la hekima lililojazwa faraja, bila hata ya kujali itikadi au chama chake cha siasa. Badala yake wameamua kutoa faraja kwa waumini wao kwa kuzingatia utashi wa kisiasa,"
alisema.
Alisema Maaskofu wameamua kutumia msukumo wa kiimani pamoja na kuzitumia nyumba zao za ibada ili kuwazuilia Waislamu wasipate haki yao ya kuwa na Mahakama ya Kadhi na kutoa madai ya 'Waislamu kupewa rushwa' ili kufanikisha mchakato wa Katiba inayopendekezwa.
Alisema madai hayo yanaonesha dharau, kiburi na kutowaheshimu waislamu jambo ambalo lina athari mbaya kwa mahusiano baina ya Waislamu na Wakristo nchini.
Shekhe Mataka alisema
Alisema Taasisi hiyo inawakumbusha Maaskofu kuzingatia kuwa madhara ya kuwagawa watanzania kwa misingi ya kiimani, dhambi yake haitoishia kwenye kadhia ya Mahakama ya Kadhi wala Katiba inayopendekezwa bali itaendelea kukita mizizi yake katika kila jambo linalowahusu watanzania.
Alisema Maaskofu wameamua kutumia msukumo wa kiimani pamoja na kuzitumia nyumba zao za ibada ili kuwazuilia Waislamu wasipate haki yao ya kuwa na Mahakama ya Kadhi na kutoa madai ya 'Waislamu kupewa rushwa' ili kufanikisha mchakato wa Katiba inayopendekezwa.
"Maaskofu wameamua kuanzisha utamaduni mpya wa kuyaendea mambo ya kisiasa kwa misingi ya kiimani na hivyo kutoa tishio la kuwagawa watanzania kwa misingi hiyo. Hivyo baada ya Taasisi yetu kujiridhisha na yaliyomo katika Tamko hilo la Maaskofu chini ya mwavuli wa TCF tunashauri hatua za kuchukua" Kwa kuwa serikali ina vyombo makini vyenye wataalamu wenye uwezo wa kufahamu na kuelewa uvunjifu wa katiba na Umoja wa Kitaifa, tunaomba ipuuze tamko hilo ambalo limeisikitisha taasisi yetu na kuwadhalilisha waislamu kwa kudai wamepewa Rushwa ya Mahakama ya Kadhi."
Alisema madai hayo yanaonesha dharau, kiburi na kutowaheshimu waislamu jambo ambalo lina athari mbaya kwa mahusiano baina ya Waislamu na Wakristo nchini.
"Suala la Mahakama ya Kadhi ni haki ya Waislamu na haliwahusu wala halihitaji ridhaa ya wasiokuwa Waislamu kama ambavyo waislamu hawajapata kuombwa ridhaa yao katika yale ambayo Serikali imekuwa ikiwafanyia wakristo na makanisa yao"
Shekhe Mataka alisema
"Taasisi hii inapinga kwa nguvu zote madai ya Maaskofu kuwa Waislamu kuwa na mahakama ya Kadhi ni uvunjifu wa Katiba, kwani sheria za Kiislamu ni moja ya vyanzo vya sheria ya Tanzania… Mahakama za Tanzania zimekuwa zikitumia sheria hizo kuhukumu kesi za waislamu kuhusu ndoa, Talaka, Mirathi toka mwaka 1963 na kufuatiwa na sheria ya Tamko la Sheria ya Kiislamu ya mwaka 1964 na kuhitimishwa na sheria ya Ndoa ya mwaka 1971".
"Jambo la msingi hapa ni kuwa kesi hizo zinahukumiwa na mahakimu wasio na elimu wala ujuzi na sifa za kuwa Makadhi kwa mujibu wa Sheria za Kiislam na ndio msingi wa Waislamu kudai uwepo wa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara".
Alisema Taasisi hiyo inawakumbusha Maaskofu kuzingatia kuwa madhara ya kuwagawa watanzania kwa misingi ya kiimani, dhambi yake haitoishia kwenye kadhia ya Mahakama ya Kadhi wala Katiba inayopendekezwa bali itaendelea kukita mizizi yake katika kila jambo linalowahusu watanzania.
"Tunawasihi watanzania wote kuendelea kudumisha undugu wao kama watanzania bila kujali rangi, dini, kabila na itikadi za kisiasa na tumkemee yeyote Yule anayetaka kutugawa kwa kutumia misingi ya kidini, kikabila, kisiasa na kiuchumi"
Akizungumzia kuhusu hali ya usalama wa nchi, viashiria vya ugaidi na mauji ya Albino, Sheikh Mataka alisema Taasisi hiyo inawakumbusha watanzania kuwa suala la kulinda na kudumisha amani na utulivu nchini ni wajibu wa kila mtanzania na kuwaomba kutoa ushirikiano kwa vyombo vya uilinzi na usalama katika kuzikabili changamoto hizo.
"Ifahamike kwamba mauaji ya albino, tishio la ugaidi na uhalifu mwingine, kamwe havitoweza kukomeshwa kama hatujengi utamaduni wa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini"
"Jukwaa linasisitiza viongozi wa dini wabaki kuwa walezi siyo kuwagawa watu. Mambo ya siasa tuwaachie wanasiasa sisi tubaki na heshima yetu ya kuwa viongozi wa dini kwa sababu hata waumini wetu wanaamini tunapoongea jambo kwamba ni tamko la Kimungu na wanatakiwa kulifuata. Kwa hili hata Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameona hili lina tatizo".
Alisema.
via Lukwangule blog
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments