NA WILLIAM KAIJAGE
1. Mgogoro wa Zitto Kabwe na CHADEMA bila shaka unatokana na "struggle for power" hususan baada ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama mwaka 2009. Mengine yote yaliyotokea baada ya hapo ni yatokanayo.
2. Kufukuzwa kwake uanachama kungetokana na misconduct, basi John Shibuda angekuwa ameshavuliwa uanachama mapema zaidi.
3. Mara nyingi, adhabu kubwa anayopewa kiongozi wa chama cha siasa huwa ni kuondolewa uongozi na kubaki na uanachama wa kawaida ambao hauna impact kubwa. Ndio maana ukiangalia chama kama CCM tokea mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1992 utakuta amewahi kufukuzwa mtu mmoja tu mzanzibar anayeitwa Mansoor Yusuph Himid tarehe 26-Aug-2013. Wengine sana sana wanajifukuza wenyewe. Walioanzisha CCJ mwaka 2010 mpaka sasa kila mmoja ana madaraka.
4. Kujiondoka kwa Zitto CHADEMA nafanisha na kuanzishwa (Aug-2013) kwa chama cha Enonomic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema wa Afrika ya Kusini ambako kumezidi kupunguza kura za ANC (chama kikongwe zaidi Afrika) kwenye uchaguzi wa mwaka 2014 ambao kwa mara ya kwanza (tokea 1994) wamepoteza two-third ya bungeni.
5. Changamoto kubwa ya kugawana kura kutafanya kuishinda CCM kuwe ni kugumu zaidi.
6. ACT inaweza isipate kura nyingi za urais mwaka huu (2015) au wasipate wabunge wengi. Lakini wanaweza kuzidi kujijenga na kupata kura nyingi za urais na wabunge miaka mi-5 ijayo (2020) baada ya kufahamika. Ikumbukwe CHADEMA kati ya 2005-2010 walikuwa na wabunge wa-5 tu wa kuchaguliwa.
7. Ikifikia hatua hiyo (ya kugawana kura), itanikumbusha mwaka 1992 kwenye uchaguzi wa Kenya ambapo Daniel Arap Moi alikuwa rais kwa kupata ushindi kiduchu wa 36% kura nyingine wakigawana Kenneth Matiba 26%, Mwai Kibaki 19.5% na Oginga Odinga 17.5%.
8. Ni bahati mbaya kwamba mazingira haya ya Bongo yametokea ndani ya CHADEMA wenyewe. Hayajasababishwa na CCM. La sivyo ingeonekana ni mbinu ya divide-and -rule. Ni sawasawa na kujitoa kwa William Ruto kutoka ODM ya Kenya na kujiunga na Jubilee Coalition mwaka 2011 kulikopelekea Raila Odinga kupoteza watu wake muhimu wa Pentagon.
9. Kuna watu wanasema exodus hii inafanana na kuondoka kwa Dr Aman Kabourou mwaka 2006 jambo ambalo napingana nalo sana. Tofauti ni kubwa (Bokeseni Ezali). Ni tofauti na jinsi Maalim Seif alivyomfukuza James Mapalala kwenye CUF.
10. Bila shaka mpaka kufikia 28-Mar-2015 atakuwa Mwenyekiti wa ACT. Labda Kitila Mkumbo atakuwa mgombea urais (kutokana na Zitto kutofikisha umri wa miaka 40). Bila shaka wagombea wengi watakaopigwa chini UKAWA (hususan CHADEMA na NCCR-Mageuzi) watakimbilia ACT.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments