Kumekucha CHADEMA, Mwenyekiti wa Wilaya Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa BAWACHA warudi CCM.
Juliana Shonza;
"... Chama ambacho kimejengwa katika misingi ya ubaguzi na damu ya watanzania hakiwezi kudumu, kitakufa tu....ndio Kinakufa na wasituhusishe na kifo chao, wanakufa kwa Ujinga wao wenyewe..."
Nape Moses Nnauye - Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi.
Mkutano wa hadhara Mto wa Mbu, Monduli.
Tarehe 13th March 2015.
Ni siku mbili tu baada ya maneno hayo ya Nape, Nyumba ya jirani ameshatua Bundi, tena ametua kwenye kiunga cha Nyumba hiyo, Mkoani Arusha. Ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Ngorongoro ndugu Revocatus William Parapara amejiondoa kwenye Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Parapara amefanya maamuzi hayo jioni hii katika mkutano wa hadhara, eneo la Wasso, Loliondo ambao umehutubiwa na Ndugu Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM ambae anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Arusha.
Ndugu Revocatus Parapara mekuwa Kiongozi Mwandamizi wa Chadema katika wilya ya ngorongoro kwa Miaka zaidi ya 10. Na katika mkutano huo ndugu Parapara amesema hawezi kuendelea kushiriki kupanda mbegu ya ubaguzi ambayo inaendelea kumea katika Chama Chake cha zamani cha CHADEMA.
Aidha aliyekuwa Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) Bi. Elinami Limbali amekihama Chama hicho akiongozana na Mwenyekiti wake wa Wilaya na Kujiunga na Chama Cha Mapinduzi, akidai kuchoshwa na sera za kuhamasisha vurugu badala ya maendeleo zinazofanywa na CHADEMA, na kusema kuwa zinapotokea vurugu watoto na akina mama ndio hupata tabu.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments