Hardships often prepare ordinary people for an exraordinary destiny.
God Help me,you have always been there for me, since my childhood.
Najua wengi mngependa kujua nini kwa Ufupi.
Kwa kawaida nimekuwa na mazoea ya kumuandalia Dr take away ya breakfast.
Ambayo Huwa inakuwa Birika Dogo sana la vikombe kama viwili hivi vya chai na mkate aina ya bager.
Birika Hilo anaenda nalo asubuhi kazini na viungo vyote,anapojisikia njaa anatia maji na kuchemsha chai yake na kunywa.
Anapokuwa na vikao vya nje au secretariat ya Chama Chake mara nyingi Huwa simfungii kwa kukubaliana na yeye kwa kuwa katikati ya vikao hivyo wanapata bites.
Khalid Kagezi- ambae ni Mlinzi bi nafsi wa baba amekuwa akitembea na hiyo sumu nafikiri kwa zaidi ya wiki moja sasa,lengo lilikuwa kumuwekea baba katika chakula hicho nachofunga ili ijulikane Mimi ndiye muuwaji kwa kuwa ndiyo muandaaji wa chakula hicho.
Kagezi-aliandaa mazingira vizuri sana kwa mda bila Mimi kujua,alikuwa akitangaza kwa watu mbalimbali kwamba Mimi nitamuuwa Dr,amekuwa akiyasema hayo kwa wafanyakazi mbalimbali pale ofisini,hata walinzi wangu nyumbani.
Lakini alienda mbali sana na kuwaambia wachungaji kadhaa ambao alijua ninafahamiana nao.
Mchungaji moja alinipa akaniambia niwe makini japo hakunieleza ni nini.
Baba Askofu Wangu Alimuita Mume Wangu na kumwambia nimesikia Mke wako anaenda kukuuwa kwa sumu,akamwambia nimeambiwa umeshapewa taarifa.kweli iliniuma sana sana,niliwaza na kulia sana kwanini asiniite kama Mtoto wake na kuniambia na anamwambia Mume wangu nini kipo nyuma ya Pazia.Ukweli nililia sana kwa siku nne mfululizo,hata Leo bado nalia kwani ingetokea asingeniamini kwa lolote.
Mungu ndiye mpagaji wa kila jambo kwa wiki nzima sikumpa baba take away yake,naambiwa alithubutu hata kumsema sekretari kwanini siku hizi simfungii chakula katika harakati za kukuza mazingira ya kuwa Mimi na Mume Wangu ha tuko vizuri,Kumbe hakujua nilikuwa na ratiba kamili ya kazi zake na tukakubaliana nisimfungie chakula.
Jumamosi-niliamka mapema nakwenda mazoezini,kagezi alipoona nimeondoka akaenda ndani (dinning)
Bahati nzuri alikutana na mama yangu wa Kazi,akamwambia mama ameniruhusu nikanywe chai.akapita na kuelewa dinning,ukweli haijawi kutokea mlinzi yoyete kuingia dinning na kuchukua chai ambayo imeandaliwa kwa ajili ya baba,(kipindi chote cha shule watoto wako boarding)
Mama msaidizi Wangu akashtuka,lakini akamuacha akaingia kwakuwa amemwambia mimi nimemruhusu,lakini hawezi kujiuliza maana Nimetoka na kagezi akawa tayari kutimiza hadhima yake,ghafla mama akaamua kwenda dinning,Kagezi alishtuka sana na kumwaga chai chini,wakataniana na mama kulikoni?basi mama akamsaidia na kwakuwa bado tu naamini japo hatujui kwa Dakika chache alifanya nini.Kagezi ikabidi atoke nje na chai yake,ambayo pia akashindwa kuinywa,walinzi na driver wakamuuliza umeifuata ya nini.
Baba hakwenda kazini,na ikabidi wao waondoke ndipo yeye akaenda moja kwa moja kwenye Ofisi za Usalana,ambapo akaonekana na vijana Wetu,na hatimae kumuoji..................kama tulivyosikia kwenye vyombo vya habari.
kinacho niumiza leo,watu kadhaa ambao binafsi niliwaamini na kuniheshimu,wananipigia na kunipa pole na kuniambia walikwisha sikia mengi maovu juu yangu na ati mimi ninajama za kumuuwa mume Wangu!!!!!!!!!!!! Kutoka kwa Kagezi.
Najiuliza????????? Kwanini hawakusema?????
Je walisubiri Yamkute Dr waninyooshee Kidole??????
INAUMA SANA
Ushauri- tusiwe wepesi wa kusikiliza Majungu na kuyasambaza kwa kuyakuza,yatakugharimu kwani kama hutajisumbua kuujua ukweli utajitengenezea dhambi ya bure.
Najua wapo wengi leo wanaohukumu watu pasipo kuujua ukweli,
Machozi ya mtu ni sumu.
KAGEZI you will pay for my tears,Mungu Wangu yupo kazini.
Hukufikiria hata watoto ?
Thx all am free.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments