>
> UUNGWANA
> (. (Dkt.Muhammed Seif Khatib)
> Uungwana ni tabia ya mwanadamu kuukubali ukweli unapodhirika.Ni
> kuheshimu maamuzi ya wengine hata kama yataleta athari kwake kimasilahi,
> kijamii na kiuchumi.Ni kukubali kukisolewa kwa matendo yake au ya walio chini
> yake.Kukubali kuikosoa jamii inpokosa,chombo au chama chake.Ni kukiri pia kuwa mafanikio ayapatayo yameletwa na wengine wenye uwezo na mamlaka
> zaidi yake au juu yake.Uungwana siyo kinyume na utwana au ujakazi.Wala siyo
> kuvaa kanzu ya darzi, kikoi,kofia ya viua,koti la lasi,viatu vya makubadhi na
> kutafuta mwendo kwa fimbo ya henzirani.Na wala siyo kuongea kwa madaha,
> fasaha huku uzungumzaji ukiwekwa mada na shada katika kila tamko.Lakini wenye uungwana ni wachache ingawa waungwana ni wengi sana miongoni mwa jamii. Waungwana wenye hulka na silka uungwana wapo wanaodhani
> kuwa hupatikana katika mwabao pwani kwa Waswahili wavao kanzu na
> tarubush!Na kuamini mrima na bara kuwakuta ni adimu.
> Mwandiga,Kigoma Kaskazini kijana mwenye uungwana amejitokeza.Miaka
> ishirini na moja au miongo miwili alilitumikia chama chake cha upinzani kwa
> moyo wote.Wengi wamemkuta akwapokea.Wengine walitapikwa na vyama
> wengine. Wengine wamekuja bila pembe.Wengie walikuja na videvu vya mfuto
> sasa wameota ndevu,sharubu na vionjamchuzi.Wao wamegeuka kuwa wenye
> chama na waasisi hawana nafasi.Chama chake kimekuwa na kupata ummarufu ni kwa
> juhudi kubwa za uungwana wa kijana huyu.Ametembea nchi nzima, usiku na mchana
> kwaajili ya kukijenga cha na kuimarisha demokrasia nje ya chama chake ndani ya bunge
> na ya chama chake.Umaarufu umeponza! Wakubwa wakaingia hofu pale alipojarbu
> kutumia haki ya kidemokrasia ya kuomba nafasi ya uongozi ya chama chake
> anachokifia damu.Ni kosa siyo kuomba bali hata kuonesha nia.Chama chake chenye
> kubeba lakabu ya Chama cha Demkrasia ndicho cha kwanza kuviza hiyo demokrasia.
> Alipoonesha nia kutaka kushika afasi za wakubwa waliopewa na wakwe nongwa na
> usongo ukaanza.Njama zikaandaliwa za kutimuliwa.Sababu zikaengwaengwa za yeye
> kufukuzwa.Hivi kwa sababu ya uungwana wake akaona ajitetee ndani ya chama.Wapi!
> Alishindwa.Chama cha demokrasia kinakandamiza demkrasia.Muungwana huyu
> akaundiwa zengwe la kumeangamiza na kumuua kisiasa.Muungwana akawekwa kizimbani.
> Akasomewa mashitaka yake kama yale katika riwaya ya Shaaban Robert katika
> Kusadikika ya Karama na Mudir wa Sheria.Yeye ni mla rushwa namba moja kutoka
> Chama cha Mapinduzi.Hakushiriki kumfanyia kampeni mgombea Urais Padri Mwaasi wa c
> wa chama chake.Aliwapendelea wabunge wa CCM ili wakishinde chama chake.Wabunge h
> hao walimuhonga.Nani hao? Mbunge wa Mpanda,Msoma vijijini na Singida Mjini.Muungwana alikisaliti chama chake kwa kutoongeza wabunge wa chama chake
> katika majimbo ya Kigoma.Alikisaliti chama chake kwa kusema hadharani kuwa
> mahesabu ya chama chake cha Kidemokrasia hayajakaguliwa.Waraka wa kumzema
> na kumuumbua yeye umetengenezwa na usalama wa Taifa na Chama Cha Mapinduzi wakati yeye Muungwana anao ushahidi kuwa umesukwa na chama chake cha Demokrasia.
> Baada ya kusomewa mashitaka hayo akavuliwa vyeo vyote vya kichama. Muungwana
> kwa kujua kuwa chama chake ni cha Demokrasia na kutambua kuwa Tanznia inafata
> utawala wa sheria akatumia uungwana wake kwenda kudai haki Mahakamani.Lo masalale
> huko huko wakamfata kumkandamiza. Mahakama ilipolitupa pingamizi lake, chama cha
> Demokrasia kikamtimua bila kufata demokrasia.Muungwana ameoneshwa uungwana
> wake kwa pande mbili.Kwa chama chake ameamua kufata maamuzi ya kutimuliwa chama
> na ubunge baada ya kutumikia kwa miaka kumi. Ilibaki miezi mitatu amalize ubunge wake.
> Ameamua kukubali udikiteta wa chama cha demkrasia na hatakata rufaa Mahakamani.
> Yalimfika Muungwana yanafanana na ya Mbunge wa Wawi na Professa Mmoja wote
> wa chama kimoja walichofukuzwa.Mmoja alitaka Ukatibu Mkuu na mmoja alitaka
> Uenyekiti wa Taifa.Kwa kutamani tu ni kosa.Uungwana na kukubali yaishe.Upande wa
> pili wa uungwana wake pale aliposimama hadharani na kuwashukuru wapiga kura wake.
> Si hayo tu. Alielezea mafanikio makubwa katika jimbo lake la Mkoa wa Kigoma.Bila
> kutafuna maneno na kumunyamunya alithibitisha Kigoma aliyeikuta sivyo ilivyo leo.
> Maeendeleo makubwa ya miundombinu hasa barabara.Daraja kubwa limefungua
> mkoa.Mtandao wa umeme umeiweka Kigoma ipo kweupeni. Uwanja wa ndege umejengwa.Muungwana huyu anajua kuwa mambo yote hayo mazuri yanatokana na
> sera inotekelezwa ni ya Chama cha Mapinduzi si ya chama chake kilichomfukuza.Na
> kwamba chama cha Mapinduzi na serekali yake haibagui kupeleka maendeleo hata
> kama majimbo yanayoshikwa na upinzani.Kwngu mimi kukubali yaishe na chama chake
> cha udikteta ni Uungwana.Kwangu mimi kuungama kuwa maendeleo makubwa
> yamepatikana Kigoma kupitia sera za Chama cha Mapinduzi na usimamizi wa serekali
> yake huo ni uungwana.Waswahili husema ' Uungwana ni vitendo na kauli siyo nasaba'.
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments