[wanabidii] UVCCM Mkoa wa lindi walaani mauaji ya Albino na kumpongeza Mhe Rais kwa Uteuzi wa Wakuu wa wilaya.

Sunday, February 22, 2015
TAARIFAKWA UMMA


Baraza Kuu laJumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa waLindi chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Amir M. Mkalipa, wamefanya kikaocha kikanuni leo tarehe 21 feb 2018, katika ukumbi wa mikutano waofisi kuu ya CCM Mkoa wa Lindi, iliyopo Wailes, Lindi mjini.


Pamoja na kujadilihoja zingine zinazohusu uimara wa jumuiya mkoani Lindi, changamoto zaVijana na Walimu, suala la migomo ya wafanyabiashara, na kuwatakawatendaji wa Serikali kutimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu ilikuongeza ufanisi wa Serikali katika kutatua kero za wananchi nakuleta maendeleo ya jamii, lakini pia kikao hicho kimeazimia:-


a} Baraza kuu laUVCCM Mkoa wa Lindi imeitaka Serikali kuendelea kuchukua hatua kalikwa watakaobainika kuhusika na mauaji ya Albino. Ni lazima Serikalikushirikiana na wananchi wahakikishe ndugu zetu Albino wanaishimaisha yenye usalama, amani na furaha kwani ni haki yao kikatiba.


b}Pia, Baraza Kuu laUVCCM Mkoa wa Lindi linampongeza Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM nduguJakaya Kikwete kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM (2010-2015) kwakukamilisha ujenzi wa barabara ya Kibiti-Mingoyo,


Pia inampongeza MheRais Jakaya Kikwete kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya yaAfrika Mashariki.


Lakini pia, UVCCMinampongeza na kumuunga mkono Mhe Rais kwa uteuzi wa wakuu wa wilayawapya 27 ambapo baadhi ya wateule hao wanatoka kwenye jumuiya hiyo,jambo ambalo ni heshima kubwa kwa UVCCM, na kudhihirisha kuwa jumuiyahiyo inatimiza wajibu wake wa kuwa tanuru la kuoka viongozi wenyeuwezo, waadilifu na wenye kuaminika katika jamii. Pia UVCCMimewapongeza ndugu Mboni Mhita na ndugu Paul Makonda kwa kuteuliwakuwa wakuu wa wilaya na kuwataka wakatimize wajibu kwa kuwatumikiawananchi kwa uadilifu na ufanisi.


Pia, UVCCM Lindiinampongeza Kamanda wa Vijana Mkoa Mhe Bernard Membe-Mbunge wa Mtamana Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa kuwa karibuna Vijana na kuiwezesha jumuiya kutimiza majukumu yake.


C} Mwisho, UVCCMMkoa wa Lindi inahimiza Halmashauri za wilaya kutenga asilimia 10% yaMapato yake kwa ajili ya maendeleo ya Vijana na Wanawake, ili vijanawanufaike kwa mikopo na waweze kujiajiri ili kukabiliana na tatizo laajira na umasikini. Jambo hili lipo kisheria sio ombi, hivyowatendaji husika wa Serikali wahakikishe wanatimiza wajibu waoipasavyo ama UVCCM itawalazimisha kutimiza wajibu huo.


Jumuiya ya Umoja waVijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi, wamepitisha ratiba yashughuli zao kwa Mwaka 2015 na wataanza ziara ya kutembelea Vijanakatika wilaya zote sita (6) za Mkoa wa Lindi.


Imetolewa na:-


….........................
SAID Y.GOHA
KATIBU WA UVCCMMKOA, LINDI

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments