TAARIFA KWA UMMA.
SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM-SO) YAKANUSHA KUMPIGIA DEBE LOWASA.
Serikali ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFMSO), kupitia msemaji wake mkuu ambaye ni Rais wa Serikali ya wanafunzi, ndugu Clinton Boniface inakanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la NIPASHE toleo namba 0578395 la tarehe 19/02/2015, lenye kichwa cha habari "WANAFUNZI WA IFM WAMTAKA LOWASA URAIS" na kwamba habari hizo hazijatolewa na uongozi wa IFMSO, wala hakuna mkutano wowote uliofanyika katika eneo la chuo cha usimamizi wa fedha kati ya waandishi wa habari na uongozi wa serikali ya wanafunzi na kutoa tamko hilo. Pia, kulingana na Katiba ya IFMSO kifungu namba 3, ibara ndogo ya 1, Katiba inakataza serikali ya wanafunzi (IFMSO) kushiriki katika mambo yoyote ya kidini au kisiasa, hivyo basi IFMSO inasikitishwa na taarifa hizo na inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na taarifa hizo.
Imetolewa na;
…..........
Clinton Boniface.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi.
IFM-SO
19/02/ 2015.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments