Ilikuwa ya pata saa 10:15 jioni nikiwa ndani ya bus la Dar Express #97909 lililotoka Karatu kwenda Dar nimekerwa na tabia ya wafanyakazi was hili bus (dereva na condakta).
Kama utaratibu wao waligawa maji na vinywaji kwa abiria na wakaweka vyombo vya kukusanyia uchafu mapema kabisa baada ya kutoka njia panda ambapo abiria walinunua chakula.
Tulipofika Mbwewe dereva akasimamisha gari na msaidizi wake akasema "Kuchimba dawa". Watu wakashuka na condakta akabeba container mbili zilizojaa uchafu wa chupa za maji, soda na aluminium foils za chakula akamwaga kwenye majani pembeni mwa barabara. Nikamwambia usimwage huko uchafu hapo. Akaniuliza " nikamwage wapi?" Nikamwambia fikisha mwisho was safari kama hamna utaratibu mwingine. Wala hakusikiliza na support ya dereva wake wakaacha ule uchafu uliotolewa ndani ya bus pale Mbwewe, zaidi ya uchafu mwingine wa vinyesi na mikojo.
Hii inaonyesha wafanyakazi wa hili bus hawana elimu ya mazingira hata ile mtu anazaliwa nayo ambayo haiitaji kufundishwa darasani.
Mwajiri wa hawa wafanyakazi anatakiwa kuelimisha wafanyakazi wake kila anapoajiri wapya. Pia itolewe elimu kwa abiria wanaorusha uchafu madirishani.
Jamani tutafika kama mpaka sasa hatubadiliki lamina na juhudi zote zinazotolewa hata kwa vyombo vya habari?
Tunaomba vyombo husika (NEMC?) vikumbushie na kuwawajibisha watu kama hawa wanaorudisha nyuma maendeleo.
--Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments