[wanabidii]

Sunday, January 04, 2015
>
> MSIMU.
> (Dkt.Muhammed Seif Khatib)
> Msimu ni kipindi maalum katika mwaka ambapo hali ya hewa mahususi au
> jambo fulani ama maalumu hujiri.Wakati mwengine Msimu hulinganishwa na
> Majira kimaana.Lakini muda maalum unaopangwa unaweza kuita majira ya
> kitu fulani.Hata maumbile ya pepo,mvua, mazao huweza kuitwa msimu au
> majira ya kitu au mazao.Hivi kwa kutambua kuwepo kwa Msimu au Majira mwanadamu
> hujipanga kukabilia na mabadiliko hayo na athari zake. Anayepuuza changamoto hizo
> atalazimishwa na mabadiliko yanayotarajiwa..Wakulima wenye busara kwa kawaida
> hujiandaa na msimu wa mvua kama za Masika au Vuli.Wavuvi hujua msimu wa
> pepo za Kusi na Kaskazi.Wafugaji hujihadhari athari za Kaskazi na kuadimika na
> malisho.Hata wanyama mbugani huhamahama kufatana na nguvu za Msimu na Majira.
> Mwaka 2015 hapa Tanzania ni msimu wa homa.Homa ni joto kali mwilini linalosababi
> shwa na maradhi anuwai.Homa huanza kuwaathiri walengwa kidogokidogo.Siyo malaria
> wala kichomi.Homa huanza kumsumbua muathirika polepole.Kadiri muda unavyosonga
> mbele ndipo homa inavyopanda.Ni MSIMU wa homa za siasa.Waathirika siyo tu
> wanasiasa bali pamoja na wakereketwa,wafurukutwa na wapigadebe na mapipa.Wapo
> wengine siyo wanasiasa lakini chapuo za msimu zikipigwa nao huenda ngowe.Joto ya
> homa mwanasiasa ya mwezi Januari linapimika na linastahamilika.Tofauti ukifika mwezi
> wa Septemba na Oktoba mwaka huu.Homa inatesa.Anayeumwa hutenda mambo ambayo
> si kawaida.Wagonjwa hawa wanafanana mambo yao wakiwa katika vyama vya
> upinzani au chamatawala.Itikadi za vyama hazitibu wagonjwa hawa waathirika.Wote
> hufanana viroja na vituko vyao.Wale wanasiasa waliomo katika madaraka na wale
> walio nje ya ulingo lakini wanamendea nafasi wote huwa wagonjwa.Ugonjwa wao ni
> kusaka madaraka. Zipi ishara za kuumwa kwao? Zipi?Hufunga safari ya kuwatembelea
> wagonjwa maalum siyo kila mgonjwa.Hawendi na madakitari, wauguzi wala madawa.
> Huko picha hupigwa ili nao waonekane watu wenye huruma na kujali watu.Kama
> hilo halitoshi,wazee mashuhuri wastaafu hutafutwa kwa udi na uvumba.Huwaendea huko
> huko walipo bila kujali sitara na faragha ya maisha .Anaishi wapi na vipi siyo muhimu.
> Akimwona na 'kumjulia hali na pia kumtakia 'maisha marefu'.Atajifanya mtu anomjali
> mstaafu .Atamsifu na kumtukuza!Atajaribu kuonesha kiasi
> gani anamuhishimu.Mwisho atamwomba 'busara na hekima' zake ili zimeongoze katika mbio
> zake.Akimwona dhaifu atamkunjia chochote na kumwachia huku akitabasamu. Mara
> nyingi mkutano huo huwa ndiyo wa mwanzo na mwisho.Hamtafuti tena.Nyakati za sikukuu
> wagonjwa hawa huhaha kutuma zawadi.Kwa watu wa mjini huwazawadia kadi,maua nachupa za mvinyo. Wengine hupelekewa bahasha zenye ukubwa tofauti na hata viwango.Huko vijijini au katika miji kwa watu wachochele kadi
> hazina uzito lakini mishiko ndiyo mipango.Wakati mwengine mitandao ya simu utaona
> zinapishana kiganjani zikikumtakia kila mtu maisha marefu na sikukuu.Hivi kwa nni ujumbe
> huo uje leo na siyo mwaka jana?Msimu wa homa ukifikia mwisho hakuna akujuaye
> si kwa hiki au kile.Waisilamu kwa mwezi huu humkumbuka Mtume au Nabii wao na huwa
> na visomo na dua zao.Wagonjwa hawaachi kushiriki katika kila kisomo.Akialikwa
> asipoalikwa atahudhuria.Atatoa michele,nyama ,tende na haluwa katika
> shughuli hiyo isomuhisi ndewe wala sikio.Harusi katika mitaa huhudhuriwa na wagonjwa
> hawa bila kupata mwaliko.Huchangia kila harusi hata bila kuombwa,Misiba ikisibu wagonjwa wa uchaguzi huikimbilia.Wenye maiti wakilia wao hupaza zaidi sauti zaidi ya
> wafiwa.Penye daftari la kuchangia, wagonjwa hawa hawasubiri kupewa hulidai
> akifika tu.
> Ziara za kutembelea maeneo hufufuka upya.Kila kukicha yupo mitaani na vijijini.
> Akipita vijiweni hasiti naye kubarizi.Akikumbana na maskani hasiti kuweka tako lake
> chini.Akiona wacharaza karata hukunja goti na kuzicharaza husemi mshabiki mzoefu.
> Huko vijijini akiona wakulima wanapiga makoongo naye hasubiri kukaribishwa atashika
> jembe na kuingia kazini.Akiona wachuma korosho atawaunga mkono au wavuna
> karanga atapinda kiuno.Mgonjwa atashiriki katika kila jambo analoliona hata kama
> hana uzoefu nalo.Mwenendo huu wa atakuwa nao kuanzia sasa hadi Oktoba.Ataongea
> na kila mtu.Atacheka na kila kiumbe.Ngoma ikipita madhali inachezwa katika eneo lake
> la kugombea uchaguzi hata ngoja akaribishwe ataingia ngomani na kudemka.Kuweza
> kufatilia midundo na mikogo kwake siyo muhimu.Yeye atakacho ni anaonekane kuwa
> mtu wa watu katika jamii.Kama ni anayepanda gari ataacha.Atapiga kwata za
> miguu na kuzunguka mitaani.Hataacha kwenda mitaani katika magenge ya mamalishe
> na kupata msosi wake huko.
> Siku nenda siku rudi vituko na viroja huzidi.Siku za kampeni mambo hupamba moto.
> Joto la homa huzidi.Mwili husinyaa kwa machofu.Wasiwasi na shauku humfanya
> asawijike.Huyu mgonjwa wa uchaguzi endapo atashinda au atashindwa homa yake
> atapona siku hiyo hiyo.Atabadilika na kuacha vituko na viroja.Atakuwa hawajui tena
> watu.Si mtu wa msaada.Hendi harusini hendi msibani.Hajui wagonjwa wala wenye shida.Hashiki jembe hakamati panga.Si wa kusuka wala kunyoa.Gari
> lake hulirudia.Ndani viyoyozi huvifungua na viyoo hufunga.Yeye huwaona
> awapitao lakini yeye haonekani.Kuwe na mvua au jua miwani ya kiza haimtoki. Mitaani ni vijijini huhama na kurudi mjini na kuendelea na hamsini zaka bila
> kuaga.Mtamwona tena miaka mitano ijayo mwaka 2020 panapomajaaliwa
> Msimu ujao!
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> O
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments