[wanabidii] VIONGOZI NA WAFUASI WA CHADEMA WAONYWA JUU YA MATUMIZI MABAYA YA WIMBO WA TAIFA

Thursday, January 15, 2015

VIONGOZI NA WAFUASI WA VYAMA VYA SIASA WAONYWA JUU YA MATUMIZI MABAYA YA WIMBO WA TAIFA-KILOMBERO.

Viongozi na wafuasi wa vyama vya siasa wameonywa juu ya matumizi mabaya wa wimbo wa Taifa kwa kuwa hiyo ni miongoni mwa alama muhimu yenye heshima Kitaifa na Kimataifa.

Hiyo inafuatia kitendo cha hivi karibuni cha wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kata ya Mchombe Wilayani Kilombero kutumia wimbo wimbo huo katika kile kinachodaiwa kinyume na utaratibu.

Hali hiyo imejitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi kwa kuwachagua ambapo kupitia sauti ya wimbo huo wa Taifa walikuwa wakiingiza maneno yanayokihusu chama chao.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wameonya kwamba halipaswi kuendelezwa kwa madai kwamba huko ni kudhalilisha alama hiyo muhimu ya Taifa.

Wananchi hao wamesema inasikitisha kuona kuwa viongozi wa chadema kata na Wilaya walikuwa wakiongoza zoezi hilo linalopaswa kukemewa.

Akitolea ufafanuzi Katibu mwenezi wa chama hicho kata ya Mchombe Bwana Expedito Kisweka amekiri kutumika kwa sauti inayofanana na ile ya wimbo wa Taifa katika wimbo waliouimba siku hiyo lakini hawakulenga kwa namna yoyote kuudhalilisha wimbo huo wa Taifa.

Ikumbukwe miaka michache iliyopita Wizara ya Elimu na Utamaduni ilipiga marufuku matumizi holela ya wimbo wa Taifa .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments