[wanabidii] UKWELI JUU YA SAKATA LA RICHMOND HUU HAPA

Thursday, January 08, 2015

UKWELI JUU YA SAKATA LA RICHMOND HUU HAPA.

Sakata la Richmond lilikaa kisiasa sana na watu walikuwa na visasi vyao pale Mh Lowassa hadi kesho anaamini alikuwa sahihi kwa maamuzi aliyoyafanya kama utakumbuka kipindi kile kulikuwa na matatizo makubwa ya umeme hivyo kukahitajika umeme wa dharula na ndipo richmond ilipokuja na kuanza kuzalisha umeme.

Katika ripoti ya kina Mwakyembe waliongea mengi na moja wapo ni kuwa richmond ilikuwa company hewa na wakaenda mbali kuwa Richmond ni stationary tu iliyopo kariakoo,na mwandishi mmoja wa gazeti la Tanzania Daima alithubutu kusema richmond imesimama for RICHARDMONDULI (Richard ni jina la mtoto wa mwisho wa mhe) yote hayo yakiwa katika kuuaminisha umma kuwa kisemwacho ni cha kweli lakini hayo yote wakati yakisemwa mitambo ya Richmond ilikuwa ikiendelea kupiga kazi pale ubungo.

Swali la kujiuliza company Hewa je na umeme wa richmond ulikuwa hewa pia?ikumbukwe pia baada ya lile sakata na serikali kuamua kuvunja mkataba na richmond serikali ilipelekwa mahakamani na kutakiwa kuilipa zaidi ya million mia na ushee USD.Sasa kama hii company ilikuwa hewa je kwanini serikali ikubali kulipa pesa zote hizo kwa company hewa?wananchi hatuambiwi jambo hili lakini muda ukifika itabidi lisemwe,pia mitambo ileile ya company hewa iliuzwa kwa Dowans na Dowans to Symbion power ambayo Rais Obama alipokuja Tanzania alizindua pia mitambo hiyo.

Na ikumbukwe kuwa unlike ESCROW Iliyochunguzwa na PAC kupitia taarifa za CAG na PCCB, Richmond ilikuwa kamati teule iliyoundwa na Bunge ambayo uchunguzi wake wa kupitia PCCB ulitupiliwa mbali sababu hakukuonekana any implication na binding evidence, ila mwisho wa siku Mwakyembe alitumia findings za threshold committee ya Public procurement Auditing in government sectors. Na ujanja ujanja mwingiii kumpaka matope LOWASSA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments