JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Taarifa kwa Umma
Jopo la Kimataifa Kutathmini Mwaka Mmoja wa BRN
Dar es Salaam, 13 Januari 2015
Jopo la Kimataifa la Tathmini (IRP) litakutana kwa mara ya kwanza nchini kupitia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa! (BRN). Jopo hilo litakuwa na wajumbe nane wakiwa ni viongozi na wataalamu wa fani mbalimbali duniani.
Katika tathmini hiyo wataalamu hao watatoa mtazamo huru kuhusu mfumo wa uendeshaji, utekelezaji na mafanikio yaliyopatikana. Rais Jakaya Kikwete atakuwa mwenyeji wa jopo hilo ambalo litakutana Dar es Salaam Januari 15 na 16, 2015.
Tathmini hiyo ni sehemu ya utamaduni wa BRN wa kujitathmini na ni hatua muhimu katika utekelezaji wa Mpango huo ambapo mafanikio yaliyopatikana katika mwaka wa kwanza (2013/14) yatahakikiwa ili kupata uhalisia wa takwimu zilizotolewa na mafanikio yaliyoripotiwa ili kuboresha utekelezaji wa malengo ya BRN.
Wakati wa tathmini hiyo, mawaziri wanaosimamia utekelezaji wa BRN katika sekta za awali (kilimo, maji, nishati, elimu, uchukuzi na fedha) watawasilisha mbele ya jopo taarifa za utekelezaji. Jopo linatarajiwa kutoa tathmini yake na kupendekeza namna ya kuboresha utekelezaji.
Wajumbe wanaounda Jopo la Tathmini ni:
1. Mhe. Festus Mogae, Rais mstaafu wa Botswana;
2. James Adams, Makamu wa Rais mstaafu wa Benki ya Dunia;
3. Knut Kjaer- Mwenyekiti wa taasisi ya FSN Capital Partners;
4. Lord Peter Mandelson, Mwenyekiti taasisi ya Global Counsel;
5. Linah Mohohlo-Gavana wa Benki Kuu ya Botswana;
6. Dkt. Nkosana Moyo- Mwanzilishi, Taasisi ya Maendeleo ya Nelson Mandela;
7. Dkt. Sipho Moyo, Mkurugenzi Mtendaji Kanda ya Afrika wa taasisi ya ONE; na
8. Jeffrey Sachs-Mshauri wa UN na Profesa wa Uchumi Chuo Kikuu cha Columbia.
Tutaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu tathmini hiyo kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Kwa taarifa zaidi au ufafanuzi tafadhali wasiliana na Idara ya Mawasiliano-Ofisi ya Rais, Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) kwa anuani zifuatazo:
1.Annastazia Rugaba- simu:+255 687 222 197
baruapepe: arugaba@pdb.go.tz
2. Hassan Abbasi –simu: +255 687 222 242
baruapepe: habbasi@pdb.go.tz
Imetolewa na:
Omari Issa, Mtendaji Mkuu,
Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (President's Delivery Bureau, PDB).
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments